TAKWIMU NI NGUZO NA NYENZO MUHIMU KATIKA KUPANGA MAENDELEO MBALIMBALI DUNIANI
Na,Agnes Mambo,Tanga.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amesema kwamba takwimu ni nguzo na nyenzo muhimu katika kupanga utekelezaji wa mipango mbalimbali maendeleo duniani.
Dkt Batilda aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini (NBS) ambapo alisema kwamba mabazara hayo yana maana mkubwa kwa wafanyakazi.
Alisema kwamba Serikali inatambua jukumu kubwa la (NBS) kuzalisha na kusambaza pamoja na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa takwimu rasmi kwa ajili ya kupanga utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo katika nchi.
Alisema kutokana na hilo wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa utashi wake mkubwa wa kisiasa alionao katika kuendeleza Tasnia ya Takwimu nchini na wote wameona mafanikio yake .
“Ndugu zangu tunaona kwa namna ya kipekee Serikali ya awamu ya sita imekuwa mstari wa mbele kuwezesha uzalishaji wa takwimu rasmi pamoja na matumizi ya takwimu katika mipango mbalimbali ya maendeleo na Dira bila takwimu hakuna kinachoendelea”Alisema
Dkt Batilda aliipongeza timu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa umoja na mshikamano kutokana na takwimu huanzia katika uzalishaji,uchakataji wake,uhakiki wake mpaka usambazaji wake kutokana na kwamba mtu moja hawezi kufanya pekee yake hivyo lazima wafanye kazi kwa ushirikiano.
Alisema kwamba wanaendelea kuhamasisha wenzao wajiunge kwenye vyama vya wafanyakazi hasa tughe ili waweze kuwa na kauli Moja ambayo itakuwa na maslahi mapana kwa nchi na sisi wenyewe.
Aliwataka kuhakikisha wanafanyakazi waelewe dira ya taasisi zao na mambo ambayo hawataajii kuyaona kwenye taasisi zao ikiwemo uvujaji wa siri.
“Katika mambo ambayo tunawapongeza sana NBS ni usiri mkubwa mlionao kwa kweli mnafanya kazi kubwa na sasa wanakwenda kwenye teknolojia ya habari tunaweza kuwa na usiri lakini mkaingiliwa kuna vita ya kimtandao inabidi tuendelee kujiimarisha sana kwa maana nyie ndio wabeba roho ya nchi”Alisema
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa sababu taarifa zote zipo kwao kwa hiyo wajipange na moja ya maeneo ambayo watapaleka watu wengi kusoma ni masuala ya ulinzi wa kimtandao ili kuungana na kikosi kazi cha Serikali ili kuhakikisha kwamba taarifa zinakuwa salama na hakuna jambo ambalo litaingizwa.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi (NBS) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt Amina Msengwa alimshukru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kumteua kuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali anatambua heshima kubwa aliyopewa na kuhidi kuendelea kusimamia ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa maelekezo na waledi mkubwa ili kuhakikisha majukumu ya NBS yanakwenda sambamba na kasi ya maendeleo.
Aidha Dkt Amina alimshukuru,Kamisaa Anna Makinda kwa kuendelea kusaidia katika kushauri na kusimamia mkakati wa usambazaji wa matokeo ya Sensa na tunaendelea kujivunia kutoka kwake
Alisema ofisi ya Taifa ya Takwimu wanataka kuijenga Tanzania yenye maendeleo makubwa na mafanikio kwani tumekuwa tukitekeleza sheria na kanuni zinazotuongoza uundaaji na uendeshaji wa vikao vya mabaraza la wafanyakazi .
Akizungumza katika mkutano huo Kamisa wa Sensa na Spika wa Bunge Mstaafu Anna Makinda amesema baraza la wafanyakazi ndio nguzo muhimu na nyenzo madhubuti ambayo inaunganisha wafanyakazi na menejimenti.
Kamisaa huyo amesikitiahwa na kuhudhunishwa na idadi ndogo ya wafanyakazi waliojiunga na chama hicho ambapo alitumia wasaa huo kuwataka watumishi kujiunga kwenye mabaraza hayo kutokana na uwepo wa manufaa mbalimbali.
"Lazima mtumie muda mwingi kuhamasishana kuniunga na mabaraza haya Kwani Kuna manufaa makubwa na Kila mara ninawakumbusha tunapokutana u Moja ni nguvu utengano ni udhaifu hamasishaneni Ili idadi iongezeke"alisema Kamisaa Anna Makinda.
Pia niwapongeze Kwa kuendelea kushikamana Kwa uchache wenu kwenye mabaraza lakini mmeendelea kujituma kufanya kazi Kwa weledi na mshikamano.
Comments
Post a Comment