BWANKU AWAONGOZA MAAFISA TAKUKURU MKOA KAGERA KUFUATILIA ENEO LA KIJIJI LINALODAIWA KUUZWA KINYEMELA.*

_Waambatana na Uongozi Serikali ya Kijiji, CCM, Wataalamu wa Kata na Mipango Miji. Waingia poli la kutisha kulipima._ 

Leo Jumanne Mei 20, 2025 Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) chini ya Abdallah Kihiyo wakiongozana na Maafisa wa Mipango Miji Mkoa chini ya Adolf Kasa wamefika kwenye Tarafa ya Katerero kufuatilia, kukagua na kupima eneo la kijiji cha Katoju lililopo eneo la Kyanguge, kitongoji cha Mahororo kwenye Kata ya Bujugo linalodaiwa kuuzwa kinyemela na baadhi ya Viongozi wa Kijiji cha Katoju. 

Maafisa TAKUKURU na wale wa Mipango Miji waliongozwa na Afisa Tarafa ya Katerero, Bwanku M Bwanku akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Bujugo Twino Felician, Kaimu Mtendaji wa Kata Anthony Babolio, Uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho, Viongozi wa Baraza la ardhi na wataalamu wengine ndani ya Kata.

Afisa Tarafa Bwanku baada ya kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ofisi ya Kijiji, aliwaongoza Maafisa hao wa TAKUKURU na wale wa Mipango Miji pamoja viongozi wote wa Kata na Kijiji ambapo walitembelea eneo hilo lililopo mwisho wa kijiji polini kulikagua na kulipima ili lisiweze kuvamiwa tena wala kuuzwa.

Ujio wa Maafisa wa TAKUKURU na Mipango Miji ni matokeo ya ziara ya Aprili 02, 2025 ya Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima aliyoifanya kwenye Kijiji cha Katoju kufuatilia malalamiko ya wizi wa ardhi za vijiji ambapo aliagiza TAKUKURU kuchunguza suala hilo.



 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO