MIRADI 12 TANGA YABAINIKA KUWA NA MAPUNGUFU KATI YA MIRADI 54 YA MAENDELEO TAKUKURU YABAINI.


Na,Agnes Mambo,Tanga.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tanga (Takukuru)imefanikiwa kufuatilia miradi ya maendeleo 54 yenye thamani ya shilingi Billion 240,264,703,118 Kwa kipindi Cha mwezi January hadi machi na kubaini mapungufu miradi 12 yenye thamani ya shilingi Billion 5,468,760,058 

Akizungumza na wanahabari Mkoani Tanga Mei 30/2025 Kaimu mkuu wa Tangukuru mkoa wa Tanga Mariamu Mayaya Kwanimba ya Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga Ramadhani Ndwatah.

Amesema katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo walibaini miradi yenye mapungufu  12 na kuitolea ushauri wa marekebisho.

Miradi hiyo iliyokuwa na mapungufu ilikuwa ya sekta ya Afya,Elimu,na Sekta ya Maji.

Kamanda Mayaya amesema katika ufuatiliaji wa kina kwenye miradi hiyo ya maendeleo 54 ambapo miradi 12 ilibainika kuwa na mapungufu ambapo ushuri wa marekebisho ulitolewa na hatua za marekebisho ya mapungufu hayo zimechukuliwa.

"Hivi sasa miradi hiyo Ipo katika Hali inayokidhi ubora kulingana na thamani ya fedha zinazowekezwa' Alisema Mayaya 

Amesema kwamba moja ya mafanikio ya utendaji wake kazi katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi 2025 uboreshaji mfumo wa huduma za udhibiti Taka Ngumu Jijini Tanga umedhibiti,chambuzi uliofanywa na TAKUKURU.

Amesema umesaidia mikakakati na maadhimio ya kulipwa Kwa madeni ya wadhabun,hivyo kufanya kazi ya uzoaji taka kuanza kutekelezwa Kwa ufanisi.

Alisema kwa upande wa uchambuzi wa mifumo katika kipindi hicho taasisi hiyo imefanikiwa kutekeleza matakwa ya sheria na kanuni za udhibiti taka ngumu nchini Tanzania kwa kutumia mfumo wa Punguza,Tumia Tena na Rejeleza taka (PTR) au Reduce,Re-use and Reycle (3R),

Aidha alisema katika mkoa wa Tanga mfumo huo ulianza katika kata ya Central,Chumbageni na Ngamiani Kati pamoja na utekelezaji wa sheria ya udhibiti wa taka ngumu,uchambuzi uliofanywa na Takukuru umesaidia mikakati na maazimio ya kulipwa kwa madeni ya wazabuni hivyo kufanya kazi ya uzoaji taka kuanza kutekelezwa kwa ufanisi.

Mariam alisema kwamba kwa ujumla zimefanyika chambuzi za mifumo 20 katika sekta za udhibiti take na usafi wa Mazingira,Afya,Kilimo na mapato ambapo wamefanikiwa kubaini mapungufu na kuwasilisha ripoti za chambuzi husika kwa wadau ambazo zimejadiliwa na maazimio yaliyofikiwa yametekelezwa na mengine yanaendelea kutekelezwa kwa ufanisi.


 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO