TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA


Dodoma

Imeelezwa kwamba Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imekuwa na mchango mkubwa katika serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akiwasilisha mada  katika Mkutano wa Maafisa habari wa Mikoa, Halmashauri na Taasisi za Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TARURA,Mratibu wa Mradi wa Agri-Connect Mhandisi Claver Mwinuka amesema serikali ya Awamu ya Sita imeongeza bajeti ya TARURA mara tatu zaidi ili kuhakikisha barabara za vijijini zinapitika kwa misimu yote.

“Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza bajeti ya TARURA mara tatu zaidi lengo ni kufikia asilimia 85 katika ujenzi na matengenezo ya barabara nchini.

Amesema mchango huo wa TARURA umeweza kuleta mafanikio makubwa ikiwemo uboreshaji wa barabara, ujenzi wa madaraja na miundombinu ya maji, ujenzi wa barabara za changarawe,matumizi ya teknolojia mpya ambapo barabara hizo zimeweza kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara  kufikia masoko.

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO