RAIS SAMIA ANAUFUNGUA MKOA WA KAGERA KWA MIUNDOMBINU YA KISASA INAYOPITIKA MUDA WOTE- GAVANA BWANKU.*
πAmeyasema hayo alipotembelea ujenzi wa Daraja la Kyetema linalounganisha mikoa yote nchini na mkoa wa Kagera kuelekea nchi ya Uganda kupitia Mutukula._
Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero iliyopo mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku mchana wa leo Jumatano Mei 28, 2025 ametembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa Daraja kubwa na la Kisasa la Kyetema linalogharimu Bilioni 8.5 likiunganisha mikoa yote ya Tanzania na Mkoa wa Kagera hasa Makao Makuu ya Mkoa kwenye Mji wa Bukoba hadi kuelekea nchi ya Uganda kupitia mpaka wa Mutukula.
Gavana Bwanku alipokelewa na Meneja wa TANROAD Mkoa wa Kagera Eng Ntuli John na kupata maelezo ya ujenzi wa Daraja hilo litakalokamilika Novemba mwaka huu na kuendelea kuimarisha miundombinu kuingia Mkoa wa Kagera.
Daraja hili linajengwa eneo la Kyetema, Kata ya Kemondo, Tarafa ya Katerero ambapo limebomolewa Daraja dogo la zamani lililokua limechoka na kuhatarisha usalama na sasa linajengwa hili jipya kubwa na la kisasa. Daraja hili ni muhimu sana na linaendelea kutimiza adhima ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuufungua mkoa huu wa mpakani kuwa na miundombinu imara inayopitika kila muda ili kuchochea shughuli za maendeleo za wananchi.
Afisa Tarafa Bwanku aliambatana na Mtendaji wa Kata ya Kemondo Ndugu Cyriacus Sosthenes na kukuta pia Wasimamizi wa mradi kutoka kwa Mkandarasi Kampuni ya Gemen Engineering Ltd. Mkandarasi amechepusha barabara pembeni ambapo magari, pikipiki, watu na vyombo vingine vinapita huku ujenzi ukiendelea bila changamoto yoyote ile.
Comments
Post a Comment