WATAALAM SADC WAKUTANA ZIMBABWE KUJADILI SEKTA YA NISHATI NA MAJI

📌 *Miundombinu ya usafirishaji umeme kikanda kujadiliwa* 📌 *Nishati Safi ya kupikia kupewa kipaumbele* 📌 *Mkakati mahsusi wa kuongeza watumiaji wa umeme Afrika (M300) kuwa moja ya Ajenda* 📌 *Maendeleo ya Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi pamoja na umeme vijijini kujadiliwa* Wataalam wa Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zake leo wameshiriki katika Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu na Watalaam wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji unaofanyika katika Jiji la Harare nchini Zimbabwe. Mkutano huo wa awali ni sehemu ya maandalizi kuelekea katika Mkutano wa pamoja wa Kamati ya Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huo pamoja na kujadili masuala ya Nishati na Maji, umekuwa ni fursa pia kwa Tanzania kuendeleza diplomasia ya kiuchumi pamoja na kuwasilisha mafanikio ya nchi katika kuboresha huduma za nishati vijijini kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijjni (REA). ...