WAZIRI MCHENGERWA AWAFUNDA MA RC WAPYA*


Na John Mapepele 

Mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaapisha na kutoa maelekezo kwa viongozi kadhaa aliowateua ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kuwafunda.

Mhe. Mchengerwa amewataka kuzingatia maelekezo yote waliyopatiwa na Mhe. Rais huku akisisitiza kuwa wanatakiwa kuwatumikia wananchi kwa kuwa Serikali ni ya wananchi na wasisite kuwasiliana na Wizara wapatapo changamoto.

"Ndugu zangu nadhani mmeiona dhamira ya Mhe. Rais ya kuwataka kwenda kuwatumikia wananchi.Mimi siwezi kuongeza chochote nawaombeni mkayazingatie yale yote aliyowaelekeza" amesisitiza Mhe Mchengerwa 

Katika hotuba yake baada ya kuwaapisha  Wakuu wa Mikoa hao wapya  Mhe. Rais ametoa maelekezo mahususi  manne ikiwa ni pamoja na kuwataka  kutunza amani na usalama wa  wananchi katika mikoa yao kwa kuzingatia  kuwa Tanzania inakwenda kwenye uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.  


Aidha amesisitiza kufanya usimamizi madhubuti wa fedha za Serikali  ili zitumike kwa kuzingatia thamani ya huduma au bidhaa zinazonunuliwa.

Pia amewaagiza kuhakikisha Wakuu wote wa Mikoa  nchini wanasimamiĆ  ukusanyaji wa mapato ya ndani bila kutumia nguvu. 

Aidha ameelekeka kwenda kuwasikiliza wananchi na kusimama katikati yao huku akisisitiza  kujishusha kwa  wananchi.

"Kuna fedha nyingi lakini mara nyingi  uongozi wa wananchi unafikiria  kuwekeza katika vitu vingine badala ya kuwekeza katika mahitaji  ya wananchi.Mathalan katika baadhi  Halmashauri miundombinu mibovu lakini fedha inayopatikana inawekezwa katika biashara nyingine hiyo siyo sawa". Amefafanua Mhe Rais 

Mkuu Mpya wa Mkoa wa Kigoma akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakuu wa mikoa wapya katika kikao na Waziri Mchengerwa aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Adolf Ndunguru na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI amesema  wanakwenda kusimamia  maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Rais na kushirikiana na Wizara mama ya TAMISEMI ili kuwatumikia wananchi na kuboresha maisha yao.



 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO