Kipeo Media ni chombo cha habari cha mtandaoni chenye kuleta taarifa za kina, sahihi, na kwa wakati. #KipeoOnlineMediaKilelechaHabariSahihinaBora.
RAIS DKT SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA PAMBA MKOANI SIMIYU
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Kiwanda cha kuchakata pamba cha Biosustain Tanzania Limited Meatu mkoani Simiyu tarehe 17 Juni, 2025.
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro Tarehe 7 Oktoba, 2025. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewashirikisha baadhi ya watalii katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ambapo wageni hao wameipongeza mamlaka hiyo kwa kuendelea kuboresha huduma na miundo mbinu ya utalii. Wakizungumza katika hafla iliyofanyika kwenye lango kuu la kuingia Hifadhi ya Ngorongoro eneo la Loduare baadhi ya watalii hao wamesema kuwa wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo na kusema wataendelea kuwashawishi wageni wengine kutoka nchi zao kutembelea Ngorongoro. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi anayeshughulikia Huduma za Utalii Mariam Kobelo amewahakikishia wageni hao kuwa mamlaka itaendelea kuboresha huduma zake na kwamba watafanyia kazi kwa ukaribu maoni yote yatakayotolewa na wateja ili kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuongeza wageni katika sekta ya utalii. “Tunaitumia wiki hii ya huduma kwa wateja kuendelea kupokea maoni mbalimbali ya wateja wetu,tumejipanga vizu...
NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi Na Musa Mathias, Same - Kilimanjaro. Katika msimu huu wa mitihani, upepo wa matumaini na hamasa mpya umevuma katika shule za sekondari wilayani Same mkoani Kilimanjaro, baada ya Benki ya NMB Tawi la Same kushirikiana na wadau wa elimu kuwatia moyo wanafunzi wa kidato cha nne na kidato cha pili wanaotarajia kuanza mitihani yao ya kuhitimu hivi karibuni, Kupitia tukio lililojawa na furaha na matumaini, Meneja wa NMB Tawi la Same, Bw. Saad Masawila , aliwasihi wanafunzi hao kusimama imara katika safari yao ya kielimu kwa kujikita kwenye misingi ya bidii, nidhamu na malengo thabiti . “Soko la ushindani wa kielimu limekuwa kubwa sana,” alisema Bw. Masawila kwa msisitizo. “Tunataka kuona wanafunzi wetu wengi wakifanya vizuri wapate division one , na hata kama itatokea changamoto, basi wasishuke chini ya division three . Mafanikio ni matokeo ya juhudi, si bahati.” Katika kuonyesh...
ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO. Tafadhali subscribe Youtube yetu hapa Na Musa Mathias, Same, Kilimanjaro. Kwa shamrashamra na hamasa kubwa za kisiasa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Same jana Septemba 2, 2025 kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi katika eneo la Maore, Kata ya Maore, Jimbo la Same Mashariki, wilayani Same, mkoani Kilimanjaro. Mamia ya wananchi walijitokeza kushuhudia tukio hilo lililoambatana na muziki, nderemo na hotuba za viongozi wa chama hicho. Katika uzinduzi huo, mgombea ubunge wa CCM jimbo hilo, Mhe. Anne Kilango Malecela, alitambulishwa rasmi sambamba na madiwani 14 wanaowania nafasi katika kata mbalimbali. Mgombea Ubunge Jimbo la Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malecela akihutubia wananchi walijitokeza kushuhudia uzinduzi wa kampeni jimboni humo. Akihutubia wananchi, Mhe. Anne Kilango aliahidi kuwa endapo atachaguliwa tena, kipaumbele chake kikubwa kitakuwa kuhakikisha barabara ya Mkomazi–Same yenye zaidi ya kilomita 100 inaje...
Comments
Post a Comment