SERIKALI MKOA WA KILIMANJARO KUENDELEA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO


Na Ashrack Miraji Kipeo Online 

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw.Kiseo Nzowa  ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Bw. Nzowa alitoa kauli hiyo leo Juni 16,2025 wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Manispaa ya Moshi, ambapo aliwataka wazazi na walezi kutoa taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya watoto mara yanapotokea ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wakati.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa, Bi. Pili Bayo, alisema kuwa Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali imekuwa mstari wa mbele katika kusimamia haki za watoto na kutoa elimu ya kupambana na ukatili katika jamii.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Mkoa wa Kilimanjaro, Ndg. Baraka Mduma, alishukuru Serikali na wadau wa maendeleo kwa kuanzisha mikakati madhubuti ya ulinzi wa mtoto, ikiwemo uundwaji wa mabaraza ya watoto katika ngazi ya mkoa na halmashauri.

Aidha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka tarehe 16 Juni, kwa lengo la kuhamasisha jamii kulinda na kutetea haki za watoto barani Afrika.







 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO