ZAIDI YA WATU 700 KUPATIWA MATIBABU YA MACHO RUNGWE.

OR - TAMISEMI

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Dkt.Diocles Ngaiza amesema zaidi ya wagonjwa 700 watapatiwa matibabu ya macho katika kambi ya matibabu ya wagonjwa wenye Mtoto wa jicho kwa siku Saba yanayoendelea katika Halmashauri hiyo.

Dkt. Ngaiza ameyasema hayo wakati alipotembelea kambi hiyo itakayohudumu kwa siku saba ikiwa imeandaliawa na Taasisi ya Hellen Keller kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya mahususi kwa ajili ya kufanya upasuaji wa Mtoto wa jicho na matibabu mengine ya macho.

“katika kambi hii tunatarajia kuhudumia watu zaidi ya 700 hadi sasa kwa siku hizi mbili tu, kuna wagonjwa zaidi ya 200 wamepatiwa huduma na wako safi kabisa tofauti na walivyokuja” alisema Dkt. Ngaiza.

Amesema Halmashauri pia imeiweka mikakati mbalimbali katika kupambana na changamoto hiyo ya macho ikiwa ni pamoja na kuongeza wataalamu wa macho na kununua vifaa tiba katika vitengo vya macho katika maeneo ya kutolea huduma za afya.

Aidha, amewataka wananchi mbalimbali wenye changamoto za macho kujitokeza kwa wingi katika huduma hiyo ili kuweza kutatuliwa changamoto hizo.



 

Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO