WASHIRIKA 24 NA VIKUNDI 12 WAFUNDWA KWA LENGO KUTOA HUDUMA KWENYE JAMII HUKU SERIKALI IKITAHADHARISHA NA KUONYA WALAGUZI WA ZAO LA MWANI,
Na Agnes Mambo,Tanga.
MKUU wa mkoa wa Tanga amezindua mradi wa ReSea WAZINDUA Proggramu ya stadi za ujasiliamali na ujuzi wa ndani katika uchumi wa Bluu kwenye mandhari ya Tanga na Pemba,Ili kuwawezesha Wanawake na vijana wajasiliamali ujuzi wa usimamizi wa biashara.
Serikali ya Tanzania Kwa kushirikiana na washirika wa mradi wa ReSea Mission inclusion muungano wa Kimataifa wa ufadhili wa asili (IUCN),Mfuko wa Ruzuku Kwa wanawake Tanzania (WFT_T na Ocean Hub Afrika Kwa msaada wa kutoka GLobal Afrika Canada Juni 15/2025 wamezindua mradi huo.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani wakati akizindua,amesema lengo la mradi huo ni kuwawezesha Wanawake na Vijana wajasiliamali lakini pia amezindua kambi ya siku saba ya Mafunzo ya uchumi wa Bluu Kwa Washirika 24 na vikundi 12 vya wanawake na vijana
Amesema Washirika 24 na vikundi 12 vya wanawake na Vijana kutoka Wilaya mbili za mkoa wa Tanga Pangani na Mkinga pamoja na mkoa wa Kaskazini,Kusini,Pemba(Mkoani,
Micheweni,Chake na Wete) alionya wafanyabiashara wanaotapeli wakulima wa zao la Mwani,Majongoo Bahari kuuzwa Bei ya chini ni kumnyonya mkulima.
Amesema Washirika hao Wanajihusisha na shughuli za msingi za uchumi wa BLUU kama vile ufugaji wa Majongoo Bahari,unenepeshaji wa kaa na uchakataji wa dagaa,kilimo Cha Mwani na uongezaji wa thamani wa mazo ya baharini .
"Naonya wanunuzi na walaguzi kufuata Bei elekezi badala ya kumnyonya mkulima Kwani kufanya hivyo ni kukiuka maagizo ya Serikali hivyo malufuku kumlangua mkulima tukibaini ama nikibaini hatua Kali tutazichukuwa haiwezekani mlangozi na mnunuzi kufaidika yeye nisawa na kuwavunja Moyo wakulima wa mazo baharini"Alisema Balozi Dkt Batilda.
Pia amewataka wanawake na vijana kutafuta masoko zaidi Ili kuongeza thamani ya mazo yao ya kilimo baharini ikiwemo zao la Mwani,Majongoo Bahari na unenepeshaji wa kaa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mipango ya Kimataifa Mission inclusion Genevieve Gauthier amesema uchumi wa Bluu unawakirisha fursa ya MABADILIKO ya kiuchumi Kwa ukuwaji Jumuishi na endelevu,hasa Kwa jamii za Pwani zinazotegemea rasilimali za baharini na majini .
Gauthier amesema Sekta kama vile ufugaji wa viumbe wa baharini,utalii wa Pwani usafirishaji wa Bahari,kilimo Cha Mwani na bioteknolojia ya Bahari ni muhimu katika kuchochea ustawi wa kiuchumi,ajira,usalama wa chakula na kuhifadhi wa mazingira.
Mkurugenzi huyo amesema katika kukabiliana na changamoto hizi mradi wa ReSea unaendesha Mafunzo ya siku saba Kwa Washirika 24 na vikundi 12 kutoka mkoa wa Tanga na mkoa wa Kaskazini Kusini na Mkoani Micheweni Chake na Wete ambapo wilaya nne zitanufaika na Mafunzo hayo.
Akizungumza kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake na vijana katika uchumi wa Bluu,Andreanne Martel mkurugenzi wa mradi wa ReSea kutoka Mission inclusion amesema uchumi wa Bluu wa haki unahitaji wanawake na Vijana kama washiriki wakuu.
Amesema Mafunzo hayo yanatambua mchango wao na kuwapa zana za kusukuma matokeo chanya.
Naye Kiongozi wa mradi wa ReSea Perpetua Angima amesema MABADILIKO ya kweli ya kiuchumi hufanyika pale mtu anaposhiriki kikamilifu kuwaweka wanawake na vijana wajasiriamali katika Mpango huu tunalenga kujenga Sekta ya uchumi wa Bluu Jumuishi na yenye nguvu ambayo inatoka fursa Kwa jamii zote za Pwani kustawi Kwa pamoja.
Naye Mkuu wa mkuu wa idara ya mawasiliano Tanzania Women Trust amesema mradi huu una lengo la kuwawezesha Wanawake na vijana ngazi ya jamii kuhifadhi rasilimali Bahari na uwendelezaji wa mazo ya Bahari Ili kutengeneza vikundi Bora katika jamii zao Kwani kihistoria walikuwa wako nyuma zaidi.
Alisema hatua ya kwanza ni kuwawezesha kutambua nafasi zao katika uongozi na kutunza mazingira katika maeneo yao na kujifunza stadi za uzalishaji mali kwenye Bahari zao na kuzindua kitita ambapo mradi utasaidia kuwawezesha kusimamia masilahi za wanavikundi wao.
Nao wanavikundi wamesema Hali ya soko la bidhaa za mazao ya Bahari ni changamoto kutokana wanazalisha Kwa gharama kubwa zaidi lakini wanauza Kwa Bei ya chini ikilinganishwa na gharama za hatua ya kwanza hadi ya mwisho katika uvunaji hivyo tunaomba Serikali iwabane wanunuzi na walaguzi wasituumize.
Comments
Post a Comment