WAACHENI WATOTO WAENDE SHULE, RAIS DKT SAMIA


Na John Mapepele -OR TAMISEMI 

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi nchini kuwaachia watoto wa kike kusoma  shule maalum za msingi na sekondari ambazo zimejengwa na Serikali.

Mhe. Rais ametoa kauli hiyo leo, Juni 16, 2025  Mkoani Simiyu alipozindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Simiyu ambapo amesema Serikali imejenga shule za aina kila mkoa ili kuwasaidia watoto wa kike.

Amesema Serikali imeamua kujenga shule hizo maalum za sayansi kwa watoto wa kike kwa kuwa walikuwa nyuma katika mkondo wa sayansi.


" Shule hizi zimekuja kama maalum kwa watoto wetu wa kike ili waweze kupata fursa ya kusoma masomo ya Sayansi na kuendelea na masomo ya juu". Amefafanua Mhe. Samia

Mhe Rais amesema  katika kuboresha elimu nchini imejenga miundombinu muhimu kama  mabweni,  madarasa, maabala, nyumba za walimu, viwanja vya michezo na majiko ya kisasa yasiyotumia kuni.

Aidha, amesema pia Serikali inajenga shule maalum kwa watoto wa kiume katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Simiyu ambapo amesisitiza kuwa watoto wengine ambao hawatapata fursa ya kuendelea na elimu ya juu wataweza kujiunga na  VETA.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amemshukuru Mhe Rais kwa maono yake ya uwekezaji mkubwa  katika elimu, afya, miundombinu, na utawala bora hapa nchini.

Mhe. Mchengerwa pia amemshukuru Mhe Rais kwa kuzindua Ofisi ya kisasa ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi hii leo kabla ya kuzindua shule hiyo.

Amesema zaidi ya bilioni 90 zimetumika kwa ajili ya kujenga  Ofisi za Wakuu wa Mikoa 26 hapa nchini.

Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi mbali na kuzindua miradi chini ya Wizara ya TAMISEMI  pia amezindua miradi kadhaa ya maendeleo.


 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO