DAR ES SALAAM YASHAURIWA KUJENGA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA KATIKA MUUNDO WA GOROFA– DKT.MFAUME.

OR-TAMISEMI

Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii   Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume  amesema kutokana na uhaba wa maeneo katika Jiji la Dar es Salaam ni  vyema  Halmashauri zifikirie kujenga majengo ya kutolea huduma za afya kwa muundo wa  gorofa.

Dkt. Mfaume amesema hayo wakati alipotembelea  kituo cha afya cha Kinondoni  kwenye ziara yake  ya kukagua upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika Manispaa ya  Kinondoni, Mkoani Dar  es salaam.

“Kutokana na uhaba wa maeneo kwenye Mkoa wetu ni vyema sasa tukafikiria  kujenga vituo vya kutolea huduma za  afya kwa  muundo wa gorofa hata kama tutajenga kwa awamu” amesisitiza.

Aidha, Dkt. Mfaume amevielekeza vituo vya afya vyenye mapato makubwa yatokanayo na wananchi kuchangia huduma  kutumia mapato hayo katika kutekeleza miradi mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa huduma bora kwa  wananchi ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba. 

“Niwapongeze kituo cha afya cha Bunju kwa kutumia fedha za mapato ya ndani zaidi ya Mil. 172 kununua vifaa tiba, na  nivielekeze vituo vyenye mapato makubwa pia kuiga mfano huu wa kituo cha afya cha Bunju” amesisitiza.

Ameongeza kuwa, katika kuelekea utekelezaji wa huduma ya Bima ya Afya kwa wote ni lazima vituo vyote vya afya kuwa tayari kwa ajili ya kuwahudumia wanachama hao kwa huduma mbalimbali.





 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO