MHE.MCHENGERWA ASHIRIKI KONGAMANO LA UCHUMI LA ARUSHA.*

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI,  Mhe. Mohamed Mchengerwa ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria  jukwaa la uchumi Arusha linalofanyika katika Ukumbi wa IACC Arusha.

Kongamano hili limejumuisha zaidi ya wadau 1000 kutoka maeneo mbalimbali duniani na kushirikisha mawaziri kadhaa wa sekta za tofauti.

Mwanamajumui wa Afrika Profesa Patrick Lumumba  pia amealikwa kuwa miongoni mwa watoa mada.

Jukwaa hilo limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa Mkoa huo kupata ujuzi wa namna ya kutumia fursa za uchumi zilizopo mkoani Arusha.




 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO