NAIBU KATIBU MKUU MWAMBENE AENDESHA KIKAO KAZI KATI YA SERIKALI NA UMOJA WA ULAYA

Na OR – TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Atupele Mwambene akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Adolf Ndunguru kama Mwenyekiti wa Kamati Tendaji, amefungua na kuendesha kikao kazi cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Green and Smart Cities Programme ambacho awali kilipokea taarifa ya utekelezaji wa kazi zinazoendelea na zitatolewa maamuzi katika kikao cha mwisho kinachotarajiwa kufanyika tarehe 14 Julai, 2025.

Kwa upande wa Wadau wa Maendeleo Mwenyekiti mwenza Bw. Marc Stalmans Mkuu wa ushirikiano wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki ameshiriki kikao hicho na kufurahia mipango na makubaliano baina ya Umoja wa Ulaya na Serikali ya Tanzania.

Aidha, kikao hicho kimepitisha masuala ya utekelezaji wa Mradi wa Green and Smart Cities kwa kuidhinisha Serikali ya Denmark kujiunga na Mradi huo ambapo Shilingi Bilioni 56 zinatarajiwa kupokelewa Serikalini, kuidhinisha matumizi ya fedha za mkopo wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Shilingi Bilioni 189 na kuielekeza timu ya utekelezaji iweze kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mradi.

Kikao hiki cha Kamati Tendaji kimewahusisha Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maji, Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanga na Mwanza, Watendaji kutoka Ofisi za Serikali zilizohudhuria, Wawakilishi kutoka Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar, mashirikia na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.




 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO