PILLAR FOUNDATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA


PILLAR FOUNDATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA

Na Mwandishi Wetu. 

Morogoro. 

Vijana wanaosoma tahasusi (course) mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro wanaounda Taasisi ya Pillar Foundation wametoa vifaa tiba kwa wanafunzi wenzao chuoni hapo wenye ulemavu wa viungo na wenye ualbino vikiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni saba baada ya kubaini ugumu wanaopitia kwa kukosa mahitaji yao ya uhakika.


Kwa mujibu wa Mratibu wa Pillar Foundation chuoni hapo Innocent Swebe amesema wamebaini ugumu wanaopitia wanafunzi wenzao baada ya utaratibu wao wa kutembelea vituo vya watoto yatima na waishio mazingira hatarishi na kushuhudia ugumu wanaopitia wenye ulemavu kwa kukosa vifaa tiba vya uhakika.

Amesema sasa wanaendesha Kampeni ya Viti Mwendo kuwagusa wenye uhitaji zaidi, ambapo sasa wamechangishana na kuwafikia wadau kuwashika mkono kwa ajili ya wanafunzi hawa wenye mahitaji maalum ambapo wametoa magongo ya kutembelea, mafuta ya ngozi, kofia na miwani, wakilenga kuwafikia wahitaji wapatao zaidi ya kumi na tano kupitia kampeni hiyo.

Jesca Ezekiel, Gifti Kimario na Rahel Nicholaus ni miongoni mwa waliofikiwa na msaada huu, mbali na kutoa shukrani zao, wameomba Pillar Foundation kuwagusa pia wahitaji wengine waliopo nje ya chuo hicho.





Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO