SALUM SIMBA BINGWA MCHEZO WA DRAFTI MICHEZO MEI MOSI 2025.*

OR- TAMISEMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amemkabidhi kombe la ushindi wa mchezo wa drafti mtumishi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Salum Simba baada ya kuibuka kinara wa mchezo huo kitaifa kwa upande wa wanaume. 

Ushindi huo ameupata katika Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi 2025 baada ya kushinda mchezo wa fainali hiyo na  kupeperusha vema bendera Ofisi ya Rais-TAMISEMI katika mashindano hayo. 

Rais Dkt. Samia alitoa zawadi kwa mshindi huyo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi iliyofanyika  kitaifa katika uwanja wa Bombadia mkoani Singida.

Ushindi wa Simba katika mchezo hiyo unaonesha vipaji vya mchezo walivyonavyo watumishi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI.



 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO