WIZARA YA MADINI YAHMIA RASIMI MTUMBA ,JENGLLA BILIONI 300 LATEKELEZWA

WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, amesema kuwa jumla ya Shilingi bilioni 300 zimetumika katika ujenzi wa jengo jipya la kisasa la Wizara ya Madini lililopo Mtumba, nje kidogo ya Jiji la Dodoma, ambapo sasa ofisi zote za wizara hiyo zitakuwa zikifanya kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri Mavunde amesema kuwa kuanzia sasa, wananchi wote watakuwa wakipata huduma za wizara hiyo katika jengo hilo jipya, hatua inayolenga kuboresha utoaji wa huduma na kuondoa changamoto zilizokuwepo awali.

“Leo ni siku ya kihistoria kwa Wizara ya Madini Tumeingia rasmi katika jengo letu jipya baada ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kutembelea na kuridhishwa na ukamilishaji wake. Huduma zote kwa wananchi zitapatikana hapa Mtumba,” alisema Waziri Mavunde.

Aliongeza kuwa: “Niliahidi mbele ya Kamati ya Bunge kuwa hadi kufikia Mei 15 tutakuwa tumekamilisha uhamisho huu Jengo hili litasaidia kupunguza adha zilizokuwepo awali, hususan ufinyu wa nafasi uliokuwa ukikwamisha utoaji wa huduma kwa wananchi.”

Aidha, Waziri huyo ametoa wito kwa watumishi wa wizara hiyo kuendelea kutoa huduma kwa kuzingatia weledi, uwajibikaji na nidhamu ya hali ya juu, ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa wakati na kwa ufanisi.



 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO