HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU KATIKA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO- ADOLF NDUNGURU


Na.Asila Twaha, OR - TAMISEMI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ndugu Adolf Ndunguru amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratibu Makatibu Tawala Wasaidizi Uchumi na Uzalishaji, Maafisa Mipango na Uratibu wa Halmashauri na Waweka Hazina wa Halmashauri kuhakikisha wanakuwa wabunifu na wataalamu wenye uthubutu katika kuhakikisha kila Halmashauri inakuwa na miradi ya maendeleo itakayoandaliwa na kutekelezwa kwa kuzingatia miongozo na ushauri wa kitaalamu.

Ndunguru ameyasema hayo tarehe 13 Juni, 2025 jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo kwa wataalamu hao yalikuwa yamefanyika kwa awamu mbili ampapo awamu ya kwanza yamefanyika kuanzia tarehe 3-6 Juni, 2025 na awamu  pili yalianza tarehe 10-13 Juni, 2025.

“Serikali  ina imani kubwa sana nanyinyi tekelezeni  majukumu yenu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi na muwe wepesi wa kueleza mapema changamoto kama zinatokea ili zishughulikiwe kwa wakati” amesema Ndunguru


Amewataka kwa waweka hazina wanatumia  mifumo ya ndani  kutunza namba za siri za kuingilia kwenye mfumo wa mapato, kufuatilia fedha zilizokusanywa na hazijawasilishwa benki kwa wakati, kufanya usuluhishi wa kibenki kwa akaunti zote za halmashauri na vituo vya kutolea huduma kwa wakati, matumizi ya TAUSI App (Toleo la Kiganjani) kuhakiki uhalali wa stakabadhi, vibali na leseni na kudhibiti ugawaji wa Float kwa wahasibu wa mapato na wakusanya ushuru.

Ndunguru amesema, dhamira ya Serikali ya kuanzisha na kutekeleza miradi kwa njia ya Special Purpose Vehicle (SPV) na Public-Private Partnership (PPP)  ni kuhakikisha inafanikiwa na  Ofisi ya Rais -TAMISEMI itaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa mikoa, wilaya na halmashauri kwa kuwashirikisha viongozi wa kisiasa ili kuhakikisha wanaelewa vyema malengo ya miradi hiyo ili kuondoa mwingiliano wa majukumu na hivyo kuwezesha utekelezaji wake kwa ufanisi katika maeneo yenu.

“Hakikisheni mnakamilisha uingizaji wa bajeti ya mwaka 2025/26 na bakaa ya 2024/25 katika mfumo wa malipo kwa muda uliopangwa ili kuwezesha kuanza kwa matumizi ya fedha” amesisitiza Ndunguru


Kwa upande wa Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais -TAMISEMI  Bi. Beatrice Kimoleta amemueleza Katibu Mkuu  kuwa  pamoja na  wataalamu hao kujengewa uwezo  pia wamepata fursa ya  kufundishwa mada mbalimbali ikiwemo  mada ya uandaaji wa maandiko ya miradi ya kimkakati.

Bi.Beatrice ametoa wito kwa wataalamu hao kuhakikisha kuwa mafunzo na elimu waliyoipata inafika pia kwa watumishi wanaowasimamia ili kuongeza tija katika usimamizi wa shughuli za Serikali katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo usimamizi wa ukusanyaji wa mapato, miradi  ya maendeleo na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.


 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO