NAIBU WAZIRI MKUU DKT DOTO BITEKO AMEFUNGUA MAONESHO YA UTALII KARIBU-KILLFAIR 2025


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko amefungua Maonesho ya Utalii yajulikanayo kama *KARIBU - KILIFAIR 2025* leo Juni 06, 2025 katika Viwanja vya Magereza jijini Arusha kwa lengo la kunadi vivutio vya utalii vinavyopatika Tanzania kwa washiriki kutoka mataifa mbalimbali yaliyomo ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika Maonesho hayo, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linashiriki kwa lengo la kuvitangaza vivutio vyake vilivyomo katika Hifadhi zake 21 zilizoenea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. Katika ufunguzi huo TANAPA imewakilishwa na Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara Massana Mwishawa na viongozi wengine Waandamizi  wa Shirika. 

Aidha, Wizara ya Maliasili na Utalii kama Wizara mama katika maonesho hayo iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb), Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia utalii Nkoba Mabula, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya na Viongozi waandamizi wa Chama na Serikali pamoja na wananchi.





 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO