WASIRA: VIONGOZI WANAOHUBIRI CHUKI, WAMEPIGA ‘WRONG NAMBA

’MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo watu wake wanaishi bila ya kubaguana kwa dini, rangi au kabila na kwamba hayo ni matunda yaliyotokana na kazi nzuri ya kujenga umoja na mshikamano iliyofanywa na waasisi wa taifa.

Aidha, amewataka wananchi kuwaepuka viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakihubiri kuvuruga amani, umoja na mshikamano uliojengwa na kudumu nchini tangu kuasisiwa kwake na kusema wanaofanya hivyo wamepiga ‘wrong namba’.

Ameeleza hayo leo Juni 11, 2025 alipokuwa akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha viongozi wa CCM Wilaya ya Nyasa, katika mji wa Mbamba Bay mkoani Ruvuma ambako anaendelea na ziara ya kuimarisha Chama.

“Tuna makabila 126 lakini tunazungumza lugha moja, sasa ukikuta mtu ana akili timamu tena ni kiongozi wa kisiasa anataka kubomoa umoja huu huyo mwambieni amekosea njia, mwambie umepiga ‘wrong namba’.

“Unajua unapiga halafu unaambiwa namba uliyopiga haipatikani. Sasa mwambie hapa ulipopiga ni namba ambayo haipatikani. Niwaambie mafanikio yetu kama Chama katika Afrika ni kuwaleta watu pamoja na wakaishi kama familia moja na msingi wa umoja wetu ndio siri ya amani yetu,” alieleza.

== ==


 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO