WATUMISHI TUNZENI SIRI ZA UTUMISHI WA UMMA- DKT. JINGU
WATUMISHI TUNZENI SIRI ZA UTUMISHI WA UMMA- DKT. JINGU
Na Mwandishi Wetu,
Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt John Jingu amewataka watumishi kuzingatia maadili ya kazi ikiwa ni pamoja na kutunza siri za utumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao.
"Niwapongeze kwa kuaminiwa na kupata nafasi hii adhimu, nendeni mkafanye kazi kwa bidii huku mkizingatia maadili ya utumishi wa Umma, kafuateni sheria na taratibu zilizowekwa ambazo zinaelekeza nini kifanyike na nini kisifanyike.” amesema Dkt Jingu.
Sanjari na hayo ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu imeweka mazingira wezeshi kwa watumishi wa umma ikiwemo fursa zinazotolewa na taasisi za fedha na amewasihi watumishi hao kuzitumia.
Wizara imepokea watumishi wapya 39 wakiwemo Maafisa Ustawi wa Jamii Wasaidizi 25, Mafundi Sanifu wawili, Wahudumu wa Afya wanne, Wapishi wawili, Waandishi waendesha Ofisi watatu, Afisa Hesabu Msaidizi mmoja, Afisa TEHAMA mmoja na Afisa Muuguzi mmoja.
Comments
Post a Comment