Posts

Showing posts from February, 2026

BONDE LA OLDUVAI LILIVYOMTOA BINADAMU ANAYEPAMBANA NA MAISHA KARIAKOO*

Image
Mjua kwao hapotei njia, na mwenda pole hajikwai, unaweza ukafikiri utani kumbe inaelekea ni hivyo wale wote wanaopambana Kariakoo, Gaza, Teheran na kwingineko inaaminika kuwa asili yao ni Bonde la Olduvai lililoko eneo la hifadhi ya Ngorongoro. Bonde la Olduvai linafahamika kama eneo la kipekee duniani kupatikana masalia ya jamii za binadamu wa kale na zana za mwanzo za mawe yanayowakilisha hatua muhimu za awali katika chimbuko la binadamu kuanzia miaka milioni 2 iliyopita hadi sasa.  Kupitia eneo hili ndio ulimwengu ulipoanza kujua historia ya safari ya mabadiliko ya mwanadamu baada ya ugunduzi wa fuvu maarufu la Zinjanthropus mwaka 1959 ambalo lilibadilisha uelewa na mtazamo wa wanasayansi kuhusu mchango wa Tanzania katika masuala ya asili ya binadamu. Bonde Olduvai limehifadhi visukuku, historia na chimbuko la binadamu katika mtiririko uliokamilika.

PROF. JANABI AZINDUA WODI YA WATOTO WACHANGA KWIMBA KUINUA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Image
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi, akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, amezindua  jengo maalum la kisasa la kuhudumia watoto wachanga hususan wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza Februari 28, 2026, hatua inayolenga kuinua huduma za afya ya mama na mtoto katika mkoa huo. Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Doris Mollel Foundation (DMF) kwa kushirikiana na Keep a Child Alive (KCA), likiwa na lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa watoto njiti, sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha sekta ya afya. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Prof. Janabi amesema uwekezaji huo unaonyesha dhamira ya dhati ya wadau wa maendeleo katika kuhakikisha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wanapata huduma bora, salama na zenye viwango vya kimataifa. Amesisitiza kuwa kuimarisha huduma za wat...

KASOKO YA NGORONGORO (BUSTANI YA EDEN)*

Image
Kasoko ya Ngorongoro ndilo shimo kubwa zaidi la volkano duniani ambalo halijavunjika (lipo kamili) likiwa na wanyamapori wa aina mbalimbali, Mara nyingi huitwa Bustani ya Edeni kwa kuwa eneo hilo lina mkusanyiko mkubwa  wa wanyamapori barani Afrika, ni kasoko yenye ufahari wa kipekee ambapo uhai hustawi kwa uwiano wa kipekee na wa asili.

JASI YATIKISA SAME

Image
- Wachimbaji Waanzisha Mfuko wa Ukarabati wa Mazingira - Wakusanya Shilingi Bilioni 2.6 kwa Miaka Miwili 📍Same SHUGHULI za uchimbaji wa madini ya Jasi katika vijiji vya Ruvu Jiungeni na Makanya, wilayani Same mkoani Kilimanjaro, zimeendelea kushika kasi huku wachimbaji wadogo wenye leseni zaidi ya 200 wakiungana kuimarisha uzalishaji na usimamizi wa rasilimali hiyo muhimu kwa viwanda vya saruji na bidhaa nyingine za viwandani. Wachimbaji hao wameanzisha chama chao kwa lengo la kusimamia maslahi na kuratibu uendeshaji wa shughuli za uchimbaji, hatua inayotajwa kuongeza tija, uwajibikaji na mchango wa sekta hiyo kwa wanachama pamoja na jamii inayowazunguka. Katika kipindi cha takribani mwaka mmoja, wamefanikiwa kuweka mifumo ya pamoja ya usimamizi na udhibiti wa mapato. Akizungumza wilayani humo, Mhandisi Abel Madaha, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro anayesimamia wilaya za Same, Mwanga, Hai, Rombo, Siha na Moshi, amesema pamoja na fursa za kiuchumi zinazotokana na madini ...

*MAJIKO BANIFU 6,000 KUSAMBAZWA SIMIYU*

Image
📍Simiyu Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kusambaza majiko banifu 6,236 katika Wilaya tano za Mkoa wa Simiyu, ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya nishati safi, salama na nafuu ya kupikia kwa Watanzania wote.  Majiko hayo ambayo yanatolewa kwa wanachi kwa bei ya ruzuku, yanasambazwa na Kampuni ya Geita Millenium Star Ltd, ambapo kila wilaya itapata majiko 1,247 ambayo yatagawiwa kwa wananchi. Akizungumza mara baada ya kupokea majiko hayo Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Faiza Salim ameishukuru Wizara ya Nishati kupitia REA, kwa kuleta majiko hayo kwa bei ya ruzuku. Mhe. Faiza amesisitiza majiko hayo kupelekwa zaidi katika kata zilizopo pembezoni ambazo hazikufikiwa na zoezi la usambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia LPG.  “ Tatizo kubwa la ukataji wa miti ovyo, kuharibu mazingira lipo maeneo ya vijijini, haswa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na vyanzo vingine vya nishati ya kupikia, hivyo niwaombe majiko haya yapelekwe kwa kasi uko vijijini kwani u...

*MKAA MBADALA MKOMBOZI MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA WATANZANIA*

Image
📌Ni kuelekea asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034 📍Morogoro Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia teknolojia mbalimbali ikiwemo matumizi ya mkaa mbadala unaozalishwa nchini ili kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034 kulingana na Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya nishati safi hapa nchini.  Wito huo umetolewa leo Februari 28, 2026 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu akiwa ameongoza na Menejimenti ya REA wakati walipotembelea kiwanda cha Shirika la Mzinga kujionea kuhusu uzalishaji wa teknolojia ya mkaa mbadala unaofanywa na Shirika hilo mkoani Morogoro. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Kingu ameeleza kuwa Serikali kupitia REA imehamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia katika ajenda ya Kitaifa ...

MAKAMU WA RAIS DKT NCHIMBI AWASILI KATIKA KATIKA KANISA LA HIJA KUSHIRIKI MISA TAKATIFU YA MAZISHI YA ASKOFU MKUU KARDINALI PENGO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili katika Kanisa la Hija ya Bikira Maria - Pugu Jijini Dar es Salaam, ambapo anaungana na waombolezaji kushiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya Mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Marehemu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. Tarehe 28 Februari 2026.

RAIS DKT SAMIA AKIZUNGUMZA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC)

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayemaliza muda wake, Bi. Veronica Nduva, tarehe 28 Februari, 2026 Ikulu, Jijini Dar es Salaam. Pamoja na masuala mengine, Katibu Mkuu ambaye anamaliza muda wake alimshukuru Mheshimiwa Rais na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha kuhudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

ROCK BLOCK YACHOCHEA MAPINDUZI YA UJENZI KILIMANJARO

Image
Ajira 122 zatengenezwa, Serikali yavuna Shilingi Milioni 400/- 📍Rombo, Februari 28, 2026 MGODI wa Rock Block uliopo Wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, umeendelea kuwa kichocheo cha mageuzi katika Sekta ya Madini ya Ujenzi kwa kuzalisha ajira 122 na kuiingizia Serikali zaidi ya Shilingi milioni 400 katika kipindi cha miaka mitatu ya uendeshaji wake. Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Abel Madaha, amesema hayo kupitia mahojiano maalum Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa uchimbaji na uchongaji wa miamba kwa ajili ya kutengeneza matofali na bidhaa nyingine za ujenzi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kusimamia na kuendeleza madini ya ujenzi ili kuongeza thamani na mapato ya taifa. Amesema mgodi huo umeendelea kuchangia mapato ya Serikali kupitia ada, mrabaha na kodi mbalimbali zinazolipwa kwa taasisi ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Halmashauri ya Wilaya, hali inayochochea maendeleo ya kiuchumi katika eneo la Rombo na mkoa wa...

USHAHIDI WA TUNDA LA MTI WA KATI KULIWA NGORONGORO HUU HAPA*

Image
Mwaka 1976, Mtafiti wa masuala ya Akiolojia Dr. Mary Leakey aligundua nyayo za zamadamu  eneo la Laetoli zilizohifadhika katika mwamba wa jivu la volcano iliyolipuka kwenye milima ya Ngorongoro *zaidi ya* miaka milion 3.6 iliyopita. Wataalamu wanaamini kuwa nyayo hizo ziliachwa na jamii ya watu wa kale waitwao _Australopithecus Afarensis._ Nyayo za Zamadamu Laetoli Ngorongoro ni ushahidi usiopingika kuwa zamadamu (Hominin) wa umri wa miaka milioni 3.66 iliyopita walitembea wima kwa miguu miwili eneo la Laetoli Tanzania.  Kutembea wima  kwa miguu miwili kunatutofautisha wanadamu na wanyama  kama Sokwe na Nyani waliotokana na babu/bibi mmoja  miaka *takribani* millioni 7 iliyopita. Uwepo wa *Nyayo na masalia ya* binadamu, ndege na wanyama, urithi wa utamaduni, mambo kale, mimea, maji, matunda na kila kitu kinachomfanya binadamu kuishi ni kiashiria kuwa pengine  bustani ya Eden ni Ngorongoro ni mahali ambapo tunda la mti wa katikati lililiwa.

SERIKALI YAFANYA UKAGUZI WA KIZIMBA NA KITUO CHA ASKARI KUKABILIANA NA WANYAMAPORI WAKALI BA WAHARIBIFU

Image
  Na. John I Bera, Ruvuma Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya ukaguzi wa kizimba cha mamba katika Kijiji cha Mtonya na  Kituo  cha askari katika Kijiji cha Nambecha, Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma ikiwa ni miongoni mwa mikakati inayotekelezwa na serikali katika kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.  Ukaguzi huo umefanyika tarehe 27 Februari 2026, ambapo watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, hususan Idara ya Wanyamapori kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya husika walitembelea maeneo hayo kwa lengo la kuona maendeleo ya miundombinu hiyo. Kwa upande wa wananchi ambao ni  wakazi wa maeneo husika walionesha furaha yao na kuipongeza serikali kwa juhudi za kuweka vizimba hivyo, ambavyo vimewasaidia kujikinga na madhara ya mamba pindi wanapotumia maji ya mto Mtonya kwa matumizi ya nyumbani. Aidha, wamekuwa wenye furaha, amani na kuona usalama wao kuimarishwa zaidi. Wananchi wameipongeza...

SERIKALI YADHAMIRIA KUMALIZA CHANGAMOTO YA USAFIRI DAR ES SALAAM

Image
NA. MWANDISHI WETU – Dar es Salaam KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa DART amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha inamaliza changamoto ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam, ili wananchi waweze kupata huduma bora, ya haraka na yenye uhakika. Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya usafirishaji jijini humo, Dkt. Yonazi amesema Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika kuboresha sekta ya usafiri wa umma. Alisema katika ziara hiyo, kamati ilitembelea Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) pamoja na Kampuni ya Uendeshaji wa Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na kujionea maendeleo ya uwekezaji uliofanywa “Ni dhamira ya Serikali kuhakikisha usafiri wa Dar es Salaam unakuwa bora, wa kisasa na unaokidhi mahitaji ya wananchi. Tumejionea miundombinu iliyowekwa na jitihada zinazoendelea kuboresha huduma,” alisema. Dkt....

*REA YAENDELEA NA UHAMASISHAJI MIRADI YA NISHATI VIJIJINI MARA* .

Image
📌 *Wananchi wahamasika kujiunga na huduma ya umeme* . 📌 *Wananchi waunga mkono matumizi ya nishati safi ya kupikia* . 📍 *Mara*  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea na ziara ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya umeme pamoja na matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani Mara. Uhamasishaji umehusisha utoaji wa elimu kwa wananachi namna ya kufanya maombi ya kujiunga na huduma ya umeme huku lengo kuu likiwa ni  kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme na kuwakumbusha wananchi umuhimu wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.  Aidha, Wakala umefanya Kampeni zinahusisha utoaji wa elimu kuhusu umuhimu na faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo utunzaji wa afya, mazingira pamoja na usawa wa kijinsia. Aidha, Wakala umetoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi bora  ya umeme hususani katika shughuli za uzalishaji ikiwemo shughuli za biashara, kilimo, na shughuli za nyumbani. Vile vile, Wakala umetoa elimu kuhusu taratibu rahisi za kuom...