*AFE KIPA AFE BEKI, UJENZI WA BARABARA ZA NGORONGORO HATUNA BREKI*



Hakuna kulala, ndivyo kauli ya Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Bw. Abdul-Razaq Badru baada ya kufanya ziara ya kukagua ukarabati wa barabara ndani ya hifadhi ”tutaendelea kuimarisha miundombinu yetu ya barabara yenye mtandao wa Km 646 ndani ya hifadhi kuhakikisha huduma inakuwa bora kwa watalii, wawekezaji na wananchi”

Akiwa kijiji cha Endulen Kamishna Badru amesema barabara zote kuanzia geti la Loduare hadi Golini yenye km 88, View Point hadi Naiyobi yenye Km 76, Kimba, Edulen hadi makao yenye Km 77 inayosimamiwa na TANROADS, Endulen hadi Ndutu yenye km 52, Ndutu - Golini yenye km 23, Makumbusho Olduvai kwenda Nasera yenye Km 54  na Barabara za kreta ya Ngorongoro zenye urefu wa Km 110  zitaendelea kuimarishwa na kupitika wakati wote

“Tunataka viwango vya utoaji huduma kwa wateja wetu viwe  juu,ndio maana mda wote tupo site kuhakikisha mitambo inafanya kazi na kila barabara inapitika mda wote wa majira ya mwaka" amesisitiza Kamishna Badru



Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO