Kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi vijijini yaridhishwa na ujenzi wa barabara ya Spencon–Mabogini–Kahe Chekereni
Kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi vijijini yaridhishwa na ujenzi wa barabara ya Spencon–Mabogini–Kahe Chekereni.
Na Mwandishi wetu,
Moshi, Kilimanjaro.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Moshi vijijini, mkoani Kilimanjaro imeridhishwa na ujenzi wa barabara ya Spencon–Mabogini–Kahe Chekereni yenye urefu wa kilomita 31.25 inayojengwa kwa kiwango cha changarawe, ambapo itagharimu zaidi ya Sh7 bilioni.
Kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa watumiaji wa barabara hiyo pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananachi wa kata tatu za Kahe Mashariki, kahe Magharibi na Mabogini.
Haya hivyo, leo kamati hiyo ya siasa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) imetembelea mradi huo na kukagua ambapo wamemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kwenda kwa spidi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Akizungumzia mradi huo, Katibu wa chama cha Mapinduzi(CCM), Wilaya ya Moshi vijijini, Ramadhani Mahanyu amesema wameridhishwa na mradi huo na kumtaka mkandarasi kukamilisha kwa wakati uliopangwa.
"Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi za kuteketea miradi mbalimbali katika Wilaya yetu, hili ni jambo kubwa sana la kumpongeza Rais wetu, ametuheshisha sana katika Wilaya hii,"amesema Mahanyu.
Akizungumza, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo na kusema wataendelea kusimamia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi na kwamba watahakikisha fedha zinazotolewa zinaendana na thamani ya miradi hiyo.
"Sasahivi kwenye huu mradi tupo asilimia 19 ya utekelezaji wake, sisi kama serikali tutaendelea kuhakikisha tunakamikisha mradi huo kwa wakati kwa mujibu wa mkataba unavyosema na unaendana na fedha zilizolewa,"amesema DC Mnzava
DC Mnzava amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kwenda na spidi inavyotakiwa ili kuukamilisha kwa wakati.
Naye, Meneja wa Tarura Wilaya ya Moshi, Godfrey Mbena amesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo inapita katika kata za Kahe Magharibi, Kahe Mashariki na Mabogini kutatoa fursa kwa wananchi wa maeneo hayo kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa urahisi.
"Barabara hii ina jumla ya kilomita 31.25 na inapita katika kata 3 katikati ya vijiji 12.Brabara hii ni muhimu kwa kuwa ina wakazi wengi na wanajishughulisha na shughuli za kilimo ikiwemo cha mpunga na mbogamboga na pia hutumika kufika katika huduma mbalimbali za kijamii,"amesema
Amesema "Katika mwaka wa fedha 2024/25 Tarura Mkoa wa Kilimanjaro tulipata mradi wa Sh7 bilioni toka mfuko wa barabara(Road fund) kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii yenye kilomita 31.25 inayojengwa kwa kiwango cha changarawe katika Wilaya ya Moshi."
Aidha, amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutaondoa na kupunguza maeneo yenye vikwanzo na kufanya barabara kupitika katika kipindi chote cha mwaka bila changamoto kubwa.
Mwisho.




Comments
Post a Comment