NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi Na Musa Mathias, Same - Kilimanjaro. Katika msimu huu wa mitihani, upepo wa matumaini na hamasa mpya umevuma katika shule za sekondari wilayani Same mkoani Kilimanjaro, baada ya Benki ya NMB Tawi la Same kushirikiana na wadau wa elimu kuwatia moyo wanafunzi wa kidato cha nne na kidato cha pili wanaotarajia kuanza mitihani yao ya kuhitimu hivi karibuni, Kupitia tukio lililojawa na furaha na matumaini, Meneja wa NMB Tawi la Same, Bw. Saad Masawila , aliwasihi wanafunzi hao kusimama imara katika safari yao ya kielimu kwa kujikita kwenye misingi ya bidii, nidhamu na malengo thabiti . “Soko la ushindani wa kielimu limekuwa kubwa sana,” alisema Bw. Masawila kwa msisitizo. “Tunataka kuona wanafunzi wetu wengi wakifanya vizuri wapate division one , na hata kama itatokea changamoto, basi wasishuke chini ya division three . Mafanikio ni matokeo ya juhudi, si bahati.” Katika kuonyesh...
Comments
Post a Comment