INDIA YAELEZWA TUNDA LA MTI WA KATI LILILIWA NGORONGORO



India imefikiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kupata simulizi nzuri ya Eden inayosimuliwa kwenye vitabu vya dini inayoelezwa kwamba Adam na Eva walikula tunda la Mti wa kati.

Katika maonesho ya kimataifa ya utalii yanayofanyika  India tarehe 6-7 Januari, 2026 Afisa Masoko Mkuu Michael Makombe anatoa elimu kwa washiriki kuhusu kasoko ya Ngorongoro kuwa ni Eden inayozungumzwa kwenye vitabu vya dini.

“Ngorongoro tuna amini kuwa ndiyo Eden kutokana na kuwa na vitu vyote ambavyo Mungu amevitaja katika sifa za Bustani ya Eden.

Amevitaja vitu hivyo kuwa ni mandhari ya kuvutia,wanyama na ndege, matunda ya aina zote,misitu na mimea,wadudu,maji na miamba yenye mapango yenye muundo unaomfanya binadamu aweze kuwasiliana na Mungu.

Ngorongoro yenye utajiri wa Vivutio imetambuliwa na mtandao wa World Travel Awards kama kivutio bora cha utalii kwa mwaka 2023 na 2025 vivutio ambavyo  vipo sehemu moja na hivyo kudhihirisha Eden iliyotajwa kwenye vitabu vya dini



Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO