MRADI WA KUPELEKA UMEME KWENYE VITONGOJI KUCHOCHEA UCHUMI KIGOMA*



*📌Bilioni 39.7 kupeleka umeme kwenye vitongoji 196 Kigoma*

📍Kigoma

Imeelezwa kuwa Mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 9,009 Awamu ya Pili B (HEP 2B) utakaonufaisha Wateja wa awali 290,300  katika mikoa 25 ya Tanzania Bara nchini unakwenda kuchochea shughuli za kiuchumi, Biashara na Viwanda na kuongeza Pato la Taifa.

Hayo yameelezwa leo Februari 13, 2026 na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Bw. Abbas Rugwa wakati akitambulishwa mkandarasi kampuni ya Silo Power Ltd atakayetekeleza mradi huo wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 196 kwa gharama ya shilingi bilioni 39.7 mkoani Kigoma. 

"Nimeelezwa kuwa, mradi wa HEP 2B unakwenda kuunganisha wateja wapatao 6,308. Hii inakwenda kuchochea maendeleo ya wakazi wa mkoa huu kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kufungua Viwanda na Biashara, " Amesema Bw. Rugwa

Halikadhalika, Bw. Rugwa amemtaka mkandarasi kuhakikisha anamaliza mradi huo wa kupeleka umeme kwenye vitongoji kwa muda uliopangwa ili wananchi wa mkoa huo waweze kunufaika na mradi ikiwemo kufungua shughuli za kibiashara.

Naye, Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi Mhandisi Robert Dulle ameeleza kuwa, kwa mkoa wa Kigoma  jumla una vijiji 306 ambavyo vyote vina huduma ya umeme. Aidha, Mha. Dulle ameongeza kuwa katika mradi wa HEP 2B unakwenda kufikisha umeme kwenye vitongoji vyote visivyokuwa na umeme katika Mkoa wa Kigoma.



Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO