PROF. NAGU AKUTANA NA UGENI KUTOKA SHIRIKA LA NUTRITION INTERNATIONAL



Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Prof.Tumaini Nagu amekutana na ugeni kutoka Shirika la Nutrition International.

Prof. Nagu amekutana nao leo tarehe 4 Februari, 2026 Dodoma kwa lengo la  kujadili kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuimarisha huduma za lishe nchini.

Prof. amesema, Serikali inalishukuru Shirika hilo kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na matatizo ya lishe nchini na amesema Serikali inatambua mchango wa Shirika hilo katika kuimarisha huduma za lishe.

Aidha amesema,  Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Shirika la Nutrition International katika kuimarisha huduma za lishe kwenye ngazi zote za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Nutrition International Bw. Sergio Cooper  amesema, Shirika hilo lipo tayari kuendelea kuunga mkono na kuchangia juhudi za Serikali za kuimarisha huduma za lishe  hususani katika ngazi ya Kitaifa na ngazi ya Jamii.




Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO