RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI AWASILI TANZANIA



Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, amewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania, kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Mara baada ya kuwasili, Rais Museveni atafanya mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, mazungumzo hayo pamoja na masuala mengine yatalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kukuza ushirikiano sekta muhimu za uchumi ikiwemo nishati kati ya Tanzania na Uganda,hususan Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). 

Vilevile wataangazia masuala ya kikanda na kimataifa yenye maslahi ya pamoja.




 

/>

Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO