Posts

Showing posts from March, 2026

TANZANIA NA SHIRIKA LA IFC KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA BINAFSI NA UWEKEZAJI

Image
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) zimethibitisha azma ya kuendeleza ushirikiano katika kukuza sekta binafsi, uwekezaji na uchumi endelevu kwa manufaa ya pande zote mbili. Hayo yameelezwa katika mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), na Mkurugenzi wa IFC Kanda ya Afrika Mashariki, Mary Porter Peschka, yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Kombo amepongeza mchango mkubwa wa IFC katika kuimarisha sekta ya fedha nchini, hususan kupitia usaidizi kwa benki za NMB, CRDB na NBC. Amesema ushirikiano huo umeongeza upatikanaji wa mikopo na mitaji, na kuwa msaada muhimu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. Aidha, Serikali imetambua mchango wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) katika maendeleo ya miundombinu, ikiwemo huduma za ushauri kwa miradi ya kimkakati kama mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) jijini Dar...

MRADI WA DMDP II KUJENGA KILOMITA 42.78 ZA LAMI KIGAMBONI

Image
Dar es Salaam  Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara Kilomita 42.78 kwa kiwango cha lami kupitia mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika kata za Mjimwema, Kibada, Kigamboni, Vijibweni na Somangila zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni. Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Kigamboni, Mhandisi Edgar Tumsifu ambapo amesema kuwa mradi huo unaogharimu shilingi Bilioni 110 utekelezaji wake umefikia asilimia 30 huku tayari umeshaanza kuleta matokeo kwani barabara zilizokuwa na changamoto zimeshaanza kufanyiwa kazi na zikikamilika wananchi watanufaika na miundombinu hiyo. "Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea mradi huu, TARURA Kigamboni tuna mtandao wa barabara Km 1035 kati ya hizo barabara za lami ni Km 10 lakini kupitia DMDP II imetuletea Km 42.78 kwahiyo tutakuwa na zaidi ya Km 50 za barabara za lami mpaka kufikia ...

FANYENI KAZI KWA BIDII, UPENDO NA USHIRIKIANO KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI - PROF. SHEMDOE

Image
Na OWM – TAMISEMI, Dodoma  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM– TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka watumishi wa OWM- TAMISEMI kufanya kazi kwa bidii, upendo, ushirikiano, pamoja na ubunifu katika utendaji wao ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Prof. Shemdoe ametoa wito huo jana Machi 26, 2026 wakati  akifungua  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa OWM– TAMISEMI uliofanyika  Jijini Dodoma. Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa baraza hilo litumike kama jukwaa muhimu la kuimarisha mshikamano miongoni mwa watumishi na kuleta ushirikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi. “Baraza hili lina nafasi kubwa ya kukuza upendo na ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zetu za kila siku,” amesema Prof. Shemdoe. Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kushughulikia masuala ya msingi mahali pa kazi, ikiw...

TANZANIA YAPONGEZWA KATIKA JUHUDI ZA MABADILIKO YA NISHATI MKUTANO WA ZIMEC 2026*

Image
*Kitwe , Zambia* Rais wa Jamhuri ya Zambia Dkt. Haikande Hichilema amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazofanya katika kutekeleza Ajenda ya Mabadiliko ya Nishati ( Energy transition)  Barani Afrika. Rais, Dkt. Hichilema alitoa pongezi hizo Machi 26, 2026 wakati anafunga mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Madini na Nishati (ZIMEC) uliofanyika kwa siku mbili nchini Zambia. Dkt. Hichilema alisema kuwa, Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, mkakati uliopata msukumo mkubwa kutoka kwa Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan. Rais , Dkt.Hichilema aliongeza kuwa katika ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika Tanzania inatekeleza ushirikiano wa kimkakati na Zambia kwa vitendo kupitia  sera rafiki na miradi ya miundombinu inayounganisha kanda nzima. Dkt. Hichilema alipongeza kuhusu  mpango wa wizara ya migodi na maendeleo ya madini nchini Zambia kwa kuweka lengo la uzalishaji wa tani milio...

BALOZI MTEULE MAULIDAH HASSAN AAGWA NA WAZIRI KOMBO, AAHIDI KUIMARISHA DIPLOMASIA YA TANZANIA NA OMAN

Image
Balozi Mteule wa Tanzania nchini Oman, Mheshimiwa Maulidah Hassan, amefanya ziara ya kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Waziri Kombo amempongeza Balozi Maulidah kwa kuaminiwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mchango wake alioutoa alipokuwa Msaidizi Binafsi wa Rais katika masuala ya diplomasia.  Aidha, amemsisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Oman, hususan katika sekta za biashara, uwekezaji na utalii, pamoja na kulinda maslahi ya Watanzania wanaoishi nchini humo, huku akimhimiza kutumia uzoefu wake kuendeleza uhusiano huo. Kwa upande wake, Balozi Maulidah amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa imani aliyompa na kuahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu. Amesema pia kuwa amedhamiria kuendeleza diplomasia ya uchumi na kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzani...

*KAMATI YA BUNGE YAPITISHA RANDAMA YA MADINI MWAKA 2026/27*

Image
✅️ Madini Yachangia Asilimia 57 ya Mauzo Yote ya Bidhaa Zisizo za Asili Nje ya Nchi ✅️ Makusanyo mpaka Februari 2026 Yafikia Shilingi Bilioni 880 ✅️ GST Yakidhi Vigezo Kuendelea Kuwa na Ithibati Mpaka 2029 ✅️ Waziri Mavunde Asisitiza Ununuzi wa Helikopta ya Utafiti, Mipango Iko Pale Pale 📍 Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Machi 26, 2026 imepitisha Randama ya Wizara ya Madini kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2026/27 katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma, ambacho pia kimepokea taarifa ya utekelezaji wa Wizara kwa kipindi cha Julai 2025 hadi Februari 2026 kwa mwaka 2025/26. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, ameipongeza Wizara kwa namna inavyosimamia utekelezaji wa majukumu yake yaliyopelekea kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa kufikia asilimia 12.7 katika robo ya tatu ya Julai hadi Septemba 2025, ikiwemo kuibua miradi mipya na shughuli za utafiti,...

MHANDISI MATIVILA AKAGUA MIRADI YA DMDP II, ATOA WITO UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU

Image
📌TARURA kujenga takribani Km. 250 za barabara Manispaa zote za Dar es Salaam ‎ ‎Dar es Salaam ‎ ‎Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amesema Serikali kupitia TARURA inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu mkoa wa Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wake ili idumu kwa muda mrefu. ‎ ‎Ameyasema hayo ‎wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa DMDP II katika Manispaa za Ubungo na Kinondoni, akisisitiza umuhimu wa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati ili kuboresha miundombinu na maisha ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. ‎ ‎Mhandisi Mativila alikagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ya Msumi Km 9.9 na daraja la Msumi na ujenzi wa barabara ya Goba Wakorea km 7.76 zilizopo Ubungo pamoja na ujenzi wa barabara ya Mivumoni Km 4.79 iliyopo Kinondoni ambapo utekele...

TANZANIA NA URUSI KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA TEKNOLOJIA ZA KISASA ILI KUKUZA DIPLOMASIA YA UCHUMI

Image
Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), ameshiriki katika hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Taasisi ya Innopraktika kutoka nchini Urusi yenye muunganiko wa makampuni zaidi ya 142 ya Teknolojia (High Tech companies) na Kampuni ya Gen Z Corporation Limited ya Tanzania.  Hafla hiyo imefanyika tarehe 25 Machi, 2026 katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Dar es Salaam.  Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Kombo amesema Tanzania na Shirikisho la Urusi zimejizatiti kuimarisha ushirikiano katika teknolojia za kisasa, hatua inayolenga kukuza diplomasia ya uchumi kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi wa pande zote mbili.  Aidha Mhe. Waziri Kombo amesema hati hiyo ya makubaliano imekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaendelea kuimarisha utekelezaji wa Sera yake Mpya ya Mambo ya Nje, inayolenga kukuza diplomasia ya uchumi, huku ikisisitiza umuhimu wa teknolojia na ubunifu kama vichocheo vya maendeleo end...

BARAZA JIPYA LA WAFANYAKAZI LAAGIZWA KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA OFISI

Image
Na.OWM- KAM - Dodoma Baraza jipya la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano limeagizwa kuzingatia misingi ya mahusiano mazuri mahali pa kazi, uwajibikaji na uadilifu ili kuongeza ufanisi na ustawi kazini. Akizindua Baraza hilo leo tarehe 25 Machi, 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amewataka wafanyakazi wa ofisi hiyo ameeleza kuwa vipaumbele vya Ofisi hiyo ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa sheria za kazi nchini, kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008, kuratibu mafunzo ya ukuzaji ujuzi, pamoja na kuratibu fursa za ajira kwa Watanzania nje ya nchi.  Vipaumbele vingine ni kuratibu utekelezaji wa majadiliano ya pande tatu kati ya Serikali, waajiri na wafanyakazi, kufanya mapitio ya sheria mbalimbali za kazi na hifadhi ya jamii, pamoja na kuandaa miongozo ya mahusiano kazini na kuratibu maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi). Sambamba na hayo, Waziri Sangu amezishukuru taasisi z...

TANZANIA NA BENKI YA AfDB ZADHAMIRIA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amesema Ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya maendeleo ya Afrika  (AfDB), katika miradi ya kimkakati  unaendelea kuimarika jambo linawezesha nchi kukua kiuchumi. Ameyasema hayo Machi 25, 2026 alipokuwa anapokea nakala za hati za utambulisho za Mwakilishi Mkazi  mpya wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Bi. Mary Manneko Monyau, katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Mhe. Kombo amesema miradi hiyo imejikita zaidi katika sekta za miundombinu, usafirishaji, na nishati ambazo ni uti wa mgongo wa mabadiliko ya kiuchumi nchini. Ameongeza kuwa kwa sasa Benki hiyo inafadhili miradi 27 ikiwemo  Barabara ya Mzunguko wa Nje ya Dodoma, Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR)  na Mradi wa nyaya za umeme za chini ya bahari unaounganisha visiwa vya Zanzibar, Pemba, na Mafia. Aidha amempongeza  Bi. Monya...

*MTENDAJI MKUU WMA AITAKA MENEJIMENTI KUMSAIDIA RAIS SAMIA*

Image
*WMA - DODOMA*  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Alban Kihulla amewaelekeza wajumbe wa  menejimenti ya Wakala hiyo kuwa na majadiliano ya wazi na yenye tija yanayolenga kuboresha zaidi huduma kwa wananchi hivyo kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kujenga nchi. Ametoa wito huo mapema leo Machi 26, 2026 wakati akifungua   kikao kazi cha Menejimenti kilichoketi kupitia utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2025/26 na kupitia mpango na bajeti wa mwaka wa fedha 2026/27. "Majadiliano yetu yawe ya wazi na kila mmoja atoe mchango wenye tija kwa manufaa ya Taifa letu," amesisitiza. Aidha, Mtendaji Mkuu Kihulla amewataka wajumbe wa kikao hicho kinachofanyika katika ukumbi wake wa Makao Makuu, eneo la Medeli Dodoma, kuhakikisha wanaudadavua na kuuchambua kwa kina mpango na bajeti ya mwaka wa fedha ujao ili kuwezesha utekelezaji wenye tija. Wakala wa Vipimo iko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na ina jukumu kuu la kum...

MRADI WA CERC WALETA TABASAMU KATA YA NDEMBEZI MANISPAA YA SHINYANGA

Image
Shinyanga.  Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Zege la Gagi linalojengwa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga kupitia Mfuko wa Dharura (CERC) limeondoa adha ya usafiri iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu wananchi wa Kata hiyo na maeneo ya jirani.  Daraja hilo lenye urefu wa mita 11.2 na upana mita 8.2 linajengwa kwenye barabara ya Gagi ambalo linaunganisha Kata za Ndembezi na Ngokolo  katika Manispaa hiyo. Akizungumza kwenye mahojiano maalum katika ziara ya kutembelea mradi huo, Diwani wa Kata ya Ndembezi na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Upendo John Sawa amesema kukosekana kwa daraja hilo ni kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa Kata hiyo kutokana na ugumu wa kupita katika eneo hilo hasa kipindi cha masika kutokana na kivuko cha awali kusombwa na maji. "kipindi cha masika akina mama walikuwa wanajifungulia hapa, wanafunzi kwenda shule mpaka wapatikane watu wa kuwavusha, wengine wanavushwa kwa pesa, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa na wajumbe wake walikuwa wanakaa hap...

TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA NCHI YA MSUMBIJI

Image
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi msaada wa tani 500 za mahindi kwa Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji kufuatia mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha. Msaada huo umekabidhiwa Machi 24, 2026 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Shehena hiyo ya mahindi iliwasili jijini Maputo na ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania na kupokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Msumbiji uliongozwa na  Waziri wa Mipango na Maendeleo, Mhe. Salim Cripton Valá, Akikabidhi msaada huo, Mhe. Kombo alielezea uhusiano wa karibu na wakindugu uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ulioasisiwa tokea enzi za waasisi wa mataifa hayo mawili,  Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Juliaus Kambarage Nyerere na Hayati Edward Mondlane.  Waziri Kombo alisema kufuatia udugu huo, Rais Dkt. Samia amemtuma kufikisha msaada huo ili uweze k...