*MAONESHO KATIKA KONGAMANO LA NISHATI SAFI YA KUPIKIA MOROGORO*



Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius  Ndejembi akizungumza na wazalishaji,  wasambazaji na watumiaji wa nishati safi ya kupikia katika maonesho yanayoenda sambamba na Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika leo mkoani Morogoro.

Kongamano hilo limehusisha Wizara na Taasisi mbalimbali za Umma kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za fedha pamoja na wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nishati safi ya kupikia.

Kongamano limeandaliwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi likiwa na kaulimbiu ya Kuimarisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Maendeleo Endelelevu.

Kutoka Wizara ya Nishati, Mhe. Ndejembi ameongozana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Bw.Nolasco Mlay.



Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO