KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAWASILI KUKAGUA KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TCPM – TABORA



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Subira Mgalu (Mb), imewasili katika Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM Tabora kinachomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia kampuni tanzu ya TCPM mkoani Tabora na kupokelewa na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi.

Ziara ya Kamati hiyo imeanza rasmi leo tarehe 12 Machi 2026 na itakuwa na mwendelezo katika mikoa mbalimbali ambapo wajumbe wa Kamati watakagua na kujionea miradi inayotekelezwa na Wizara ya Nishati kupitia taasisi zake katika maeneo tofauti nchini.


Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO