DKT NCHIMBI ANAWATAKIA WAISLAMU NA WATANZANIA WOTE HERI SIKUKUU YA EID EL FITRI



Nauungana na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwatakia Waislamu na Watanzania wote Sikukuu njema ya Eid el-Fitri.

Tuna wajibu wa kulinda na kuendeleza tunu njema tulizozijenga katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani; tunu za upendo, mshikamano, nidhamu na kujali wengine, ili kuimarisha umoja wa kitaifa na kuijenga Tanzania yenye maadili imara, haki na usawa kwa wote.

Katika kusherehekea sikukuu hii, tuendelee kudumisha amani, kulinda utulivu wa nchi yetu na kuenzi mshikamano wa Watanzania, tukitambua kuwa umoja wetu ni nguvu yetu na msingi mkuu wa maendeleo endelevu ya Taifa letu.

Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO