MBUNGE AGNESS AWAFIKIA WANAWAKE WA KIKRISTO KWA KUWASHIKA MKONO



Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Agnes Marwa, ameungana na wanawake wa mashirika ya Kikristo katika Musoma kuadhimisha International Women's Day kwa shangwe na mshikamano mkubwa.

Katika maadhimisho hayo yaliyowakutanisha wanawake wa Christian Council of Tanzania (CCT) pamoja na WAWATA wa Manispaa ya Musoma, Mheshimiwa Mbunge alitoa pongezi kwa wanawake kwa mchango wao mkubwa katika kuimarisha maadili ya jamii, familia na maendeleo ya Taifa.
Akizungumza katika sherehe hizo, Mheshimiwa Agnes Marwa aliwahimiza wanawake kuendelea kushikamana, kujiamini na kutumia fursa mbalimbali za maendeleo ili kujiletea ustawi wao na jamii kwa ujumla.

Katika kuonesha dhamira yake ya dhati ya kuunga mkono shughuli za wanawake na taasisi za kijamii, Mheshimiwa Mbunge alitoa mchango wa shilingi milioni 2 na laki 4 (Tsh 2,400,000) kwa ajili ya ununuzi wa tent, hatua itakayosaidia kuimarisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiroho katika Manispaa ya Musoma.

Wanawake walioshiriki maadhimisho hayo walimpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa moyo wake wa kujitoa, wakisema mchango huo ni kielelezo cha uongozi unaojali na unaosimamia ustawi wa jamii.

Sherehe hizo zilifanyika katika hali ya furaha na mshikamano, zikionesha wazi nafasi na nguvu ya mwanamke katika kujenga jamii yenye maadili, mshikamano na maendeleo. 💐


Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO