TANZANIA YAPONGEZWA KATIKA JUHUDI ZA MABADILIKO YA NISHATI MKUTANO WA ZIMEC 2026*



*Kitwe , Zambia*

Rais wa Jamhuri ya Zambia Dkt. Haikande Hichilema amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazofanya katika kutekeleza Ajenda ya Mabadiliko ya Nishati ( Energy transition)  Barani Afrika.

Rais, Dkt. Hichilema alitoa pongezi hizo Machi 26, 2026 wakati anafunga mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Madini na Nishati (ZIMEC) uliofanyika kwa siku mbili nchini Zambia.

Dkt. Hichilema alisema kuwa, Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, mkakati uliopata msukumo mkubwa kutoka kwa Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Rais , Dkt.Hichilema aliongeza kuwa katika ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika Tanzania inatekeleza ushirikiano wa kimkakati na Zambia kwa vitendo kupitia  sera rafiki na miradi ya miundombinu inayounganisha kanda nzima.

Dkt. Hichilema alipongeza kuhusu  mpango wa wizara ya migodi na maendeleo ya madini nchini Zambia kwa kuweka lengo la uzalishaji wa tani milioni 3 za madini ya shaba ifikapo  mwaka 2030.

Katika mkutano huo Naibu Waziri wa Madini nchini Tanzania Dkt.Steven Kiruswa alipata fursa ya kuwasilisha mada kuhusu kuimarisha shoroba za miundombinu ya kikanda ili kuongeza tija na ushindani wa kibiashara.


Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO