TANZANIA INAUTOSHELEVU WA CHAKULA KWA ASILIMIA 130:PROF. NDUNGURU-TPHPA.



Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru amesema kuwa Tanzania imekuwa na utoshelevu wa chakula kufikia asilimia 130 kulingana na takwimu zinavyoonesha za mwaka 2024/2025 kwani ina uwezo wa kuzalisha chakula tani milioni 23 huku TPHPA ikiwa na mchango mkubwa kufikia asilimia hizo kwa kudhibiti visumbufu ambavyo vingeweza kuathili uzalishaji wa mazao kama vile baa la panya.

Prof Ndunguru ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Machi 24,2026 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari akielezea mafanikio ya miaka 3 ya Mamlaka hiyo.

"Takwimu zinaonesha mwaka 2024/25 Tanzania imekuwa na utoshelevu wa chakula wa asilimia 130 ambapo awali ilikuwa asilimia 128 sasa imeongezeka kufikia hapa kwasababu sasa tunaweza kuzalisha chakula tani milioni 23,hivyo TPHPA ina mchango mkubwa katika kufikia hapo kwasababu sisi ndio tunadhibiti visumbufu ambavyo vingeweza kuathili uzalishaji wa mazao mfano udhibiti wa baa la panya katika vijiji,kata na Wilaya".

Aidha Mkurugenzi huyo wa TPHPA amesema kuwa katika kipindi cha miaka hiyo 3 wamefanya udhibiti wa ndege aina ya kwelea kwelea ambao walifanya uvamizi kwenye skimu kubwa za mpunga kama kule mbeya,shinyanga,kapunga,Manyara na kwingineko ambapo ndege aina ya kwelea kwelea milioni 231 walivamia mazao katika Halmashauri 23 hivyo TPHPA ilifanya udhibiti na kuokoa tani za mazao milioni 1.6 ikiwemo mazao ya mpunga,uwele na mtama.

Kwa upande wa udhibiti wa Viwavi jeshi amesema kuwa TPHPA imeweza kudhibiti kwenye hekari za mazao 219,411 katika Wilaya 49 na kwa kufanya hivyo waliweza kuokoa tani za mazao 529,347 yakiwemo mahindi kwa kudhibiti visumbufu kwa mashamba mbalimbali yakiwemo yale BBT Dodoma.

Pia amesema ili kudhibiti visumbufu Mamlaka hiyo imenunua ndege nyuki za kisasa kwaajili ya ufuatiliaji  na udhibiti wa visumbufu hivyo kwenye mazao katika mashamba ambapo kwa sasa wana wanazo ndege nyuki 21 na wako katika hatua kukamilisha ununuzi wa ndege nyuki zingine 20.

Dira na Dhima ya Mamlaka hii ni kutoa udhibiti bora wa Afya ya Mimea na Viuatilifu kwaajili ya kuwezesha biashara ya mimea na bidhaa za mimea Kitaifa na Kimataifa.


Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO