KIMBUNGA CHA IPU CHATUA NGORONGORO*



Hayawi hayawi sasa yamekuwa,hatimaye ujumbe wa mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) umetembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kushuhudia maajabu yaliyowaita.

Ujumbe huo umepokelewa na Kamishna wa Uhifadhi wa  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro bwana Abdul-Razaq Badru na kuwaeleza wajumbe hao kuwa Ngorongoro ni sehemu pekee duniani yenye ikolojia imara inayojumuisha uwepo wa wanyama aina zote, mimea, misitu, ndege, urithi na malikale.

Amesema kutokana na ikolojia yake serikali imeamua kulihifadhi eneo hilo na kutambulika kuwa ni maajabu duniani na hivyo kivutio bora cha utalii kinachovutia maelfu ya wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Baadhi ya wageni waliotembelea hifadhi hiyo wamesema kwamba kufika kwao Ngorongoro kumewapa fursa ya hisia na Ndoto kukutana na uhalisia na kufahamu maajabu ya ulimwengu hasa baada ya kushuhudia umbile ya Kreta ya Ngorongoro likiwa na wanyama zaidi ya 25,000 na spishi za ndege takribani 500.

Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani unaendelea jijini Arusha huku wageni kutoka mataifa mbalimbali wakifurahia utajiri wa urithi na utamaduni uliopo nchini.





Comments

Popular posts from this blog

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

DC Mnzava akabidhiwa hati ya Pongezi na CCM kwa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani

OFISI ZA MADINI NCHINI ZATAKIWA KUIMARISHA ELIMU YA ULIPAJI KODI*