PROF. MSOFE AVUTIWA NA MIRADI YA REA, APONGEZA JUHUDI ZA KUSOGEZA NISHATI KWA WANANCHI



πŸ“Œ*Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo atembelea Banda la REA katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani*

πŸ“Œ*Apongeza utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini*

πŸ“Tanga 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof. Peter Msofe, amepongeza jitihada za Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati inayolenga kuboresha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Prof. Msofe ametoa pongezi hizo leo, Oktoba 13, 2026, alipotembelea Banda la REA katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Tanga Mjini.

Akiwa bandani hapo, amepatiwa maelezo kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na REA, ikiwemo usambazaji wa umeme vijijini na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

REA inaendelea kutumia maadhimisho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu miradi na fursa za nishati, huku ikihamasisha matumizi ya nishati katika kuongeza tija ya uzalishaji, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Aidha, REA inawakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea banda lake ili kujifunza kuhusu huduma, miradi na fursa zinazopatikana katika sekta ya nishati vijijini.

Mwisho


Comments

Popular posts from this blog

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

DC Mnzava akabidhiwa hati ya Pongezi na CCM kwa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani

OFISI ZA MADINI NCHINI ZATAKIWA KUIMARISHA ELIMU YA ULIPAJI KODI*