TANZANIA NA ANGOLA KUFUNGUA FURSA MPYA ZA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA



Tanzania na Angola zimeazimia kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia kwa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kubaini fursa mpya za maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Dhamira hiyo imejidhihirisha katika mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. TΓ©te AntΓ³nio.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili, pamoja na kubaini fursa mpya katika sekta mbalimbali zenye manufaa kwa pande zote.

Mazungumzo hayo yanaonesha dhamira ya Tanzania na Angola ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, hatua inayolenga kufungua fursa zaidi za maendeleo na kuleta manufaa kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.



Comments

Popular posts from this blog

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

DC Mnzava akabidhiwa hati ya Pongezi na CCM kwa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani

OFISI ZA MADINI NCHINI ZATAKIWA KUIMARISHA ELIMU YA ULIPAJI KODI*