NAIBU WAZIRI MAKAMBA ASHIRIKI TANZANIA CLIMATE FINANCE ROUNDTABLE 2026



Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb), ameshiriki  katika Tanzania Climate Finance Roundtable 2026, iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimewakutanisha viongozi, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wa mazingira, kwa ajili ya kujadili fursa na mikakati ya kuongeza upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Wizara ya Nishati ni mdau muhimu katika agenda ya tabianchi, hususan kupitia juhudi za kuongeza matumizi ya nishati safi, nishati jadidifu na teknolojia rafiki kwa mazingira, sambamba na kuimarisha usalama na upatikanaji wa nishati nchini.




#KipeoOnlineMedia #Habari #Tanzania #News #Update Asante kwa kusoma Kipeo Online Media. Tembelea kipeoonlinemedia.blogspot.com kwa habari zaidi, Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa youtube.com/@kipeoonlinemedia?si=vZ45foO1hBmK1xvX karibu sana.

Comments

Popular posts from this blog

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

DC Mnzava akabidhiwa hati ya Pongezi na CCM kwa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani

OFISI ZA MADINI NCHINI ZATAKIWA KUIMARISHA ELIMU YA ULIPAJI KODI*