DC NYAMAGANA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUSAJILI BIDHAA TBS
*MWANZA -* Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Jubilate Lawuo, amewataka wajasiriamali na wafanyabiashara wa vyakula na vipodozi kuhakikisha wanasajili biashara zao kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kulinda afya na usalama wa watumiaji.
Lawuo ameyasema hayo leo wakati akifungua Kliniki ya Viwango iliyoandaliwa na TBS Kanda ya Ziwa Mashariki katika maeneo ya Soko Kuu Jijini Mwanza.
Amesema hatua ya kusajili bidhaa itasaidia kupunguza athari zinazoweza kumpata mlaji na kuhakikisha bidhaa zinazouzwa sokoni zinakidhi viwango vya ubora.
Amesisitiza kuwa wafanyabiashara wanapaswa kuzingatia usalama wa chakula na vipodozi wanavyouza.
"Tukio hili ni la muhimu sana kwa sababu linatukumbusha kuwa suala la usalama wa chakula na vipodozi si jukumu la Serikali peke yake, bali ni wajibu wa kila mmoja wetu," alisema Lawuo.
Kliniki hiyo ya siku tano inatarajiwa kutoa elimu na huduma ya usajili kwa wafanyabiashara wa maeneo ya Mwanza na vitongoji vyake.
Mwisho



Comments
Post a Comment