Posts

TANZANIA NA SHIRIKA LA IFC KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA BINAFSI NA UWEKEZAJI

Image
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) zimethibitisha azma ya kuendeleza ushirikiano katika kukuza sekta binafsi, uwekezaji na uchumi endelevu kwa manufaa ya pande zote mbili. Hayo yameelezwa katika mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), na Mkurugenzi wa IFC Kanda ya Afrika Mashariki, Mary Porter Peschka, yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Kombo amepongeza mchango mkubwa wa IFC katika kuimarisha sekta ya fedha nchini, hususan kupitia usaidizi kwa benki za NMB, CRDB na NBC. Amesema ushirikiano huo umeongeza upatikanaji wa mikopo na mitaji, na kuwa msaada muhimu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. Aidha, Serikali imetambua mchango wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) katika maendeleo ya miundombinu, ikiwemo huduma za ushauri kwa miradi ya kimkakati kama mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) jijini Dar...

MRADI WA DMDP II KUJENGA KILOMITA 42.78 ZA LAMI KIGAMBONI

Image
Dar es Salaam  Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara Kilomita 42.78 kwa kiwango cha lami kupitia mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) katika kata za Mjimwema, Kibada, Kigamboni, Vijibweni na Somangila zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni. Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Kigamboni, Mhandisi Edgar Tumsifu ambapo amesema kuwa mradi huo unaogharimu shilingi Bilioni 110 utekelezaji wake umefikia asilimia 30 huku tayari umeshaanza kuleta matokeo kwani barabara zilizokuwa na changamoto zimeshaanza kufanyiwa kazi na zikikamilika wananchi watanufaika na miundombinu hiyo. "Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea mradi huu, TARURA Kigamboni tuna mtandao wa barabara Km 1035 kati ya hizo barabara za lami ni Km 10 lakini kupitia DMDP II imetuletea Km 42.78 kwahiyo tutakuwa na zaidi ya Km 50 za barabara za lami mpaka kufikia ...

FANYENI KAZI KWA BIDII, UPENDO NA USHIRIKIANO KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI - PROF. SHEMDOE

Image
Na OWM – TAMISEMI, Dodoma  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM– TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka watumishi wa OWM- TAMISEMI kufanya kazi kwa bidii, upendo, ushirikiano, pamoja na ubunifu katika utendaji wao ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Prof. Shemdoe ametoa wito huo jana Machi 26, 2026 wakati  akifungua  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa OWM– TAMISEMI uliofanyika  Jijini Dodoma. Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa baraza hilo litumike kama jukwaa muhimu la kuimarisha mshikamano miongoni mwa watumishi na kuleta ushirikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi. “Baraza hili lina nafasi kubwa ya kukuza upendo na ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zetu za kila siku,” amesema Prof. Shemdoe. Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kushughulikia masuala ya msingi mahali pa kazi, ikiw...

TANZANIA YAPONGEZWA KATIKA JUHUDI ZA MABADILIKO YA NISHATI MKUTANO WA ZIMEC 2026*

Image
*Kitwe , Zambia* Rais wa Jamhuri ya Zambia Dkt. Haikande Hichilema amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazofanya katika kutekeleza Ajenda ya Mabadiliko ya Nishati ( Energy transition)  Barani Afrika. Rais, Dkt. Hichilema alitoa pongezi hizo Machi 26, 2026 wakati anafunga mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Madini na Nishati (ZIMEC) uliofanyika kwa siku mbili nchini Zambia. Dkt. Hichilema alisema kuwa, Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, mkakati uliopata msukumo mkubwa kutoka kwa Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan. Rais , Dkt.Hichilema aliongeza kuwa katika ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika Tanzania inatekeleza ushirikiano wa kimkakati na Zambia kwa vitendo kupitia  sera rafiki na miradi ya miundombinu inayounganisha kanda nzima. Dkt. Hichilema alipongeza kuhusu  mpango wa wizara ya migodi na maendeleo ya madini nchini Zambia kwa kuweka lengo la uzalishaji wa tani milio...

BALOZI MTEULE MAULIDAH HASSAN AAGWA NA WAZIRI KOMBO, AAHIDI KUIMARISHA DIPLOMASIA YA TANZANIA NA OMAN

Image
Balozi Mteule wa Tanzania nchini Oman, Mheshimiwa Maulidah Hassan, amefanya ziara ya kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Waziri Kombo amempongeza Balozi Maulidah kwa kuaminiwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mchango wake alioutoa alipokuwa Msaidizi Binafsi wa Rais katika masuala ya diplomasia.  Aidha, amemsisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Oman, hususan katika sekta za biashara, uwekezaji na utalii, pamoja na kulinda maslahi ya Watanzania wanaoishi nchini humo, huku akimhimiza kutumia uzoefu wake kuendeleza uhusiano huo. Kwa upande wake, Balozi Maulidah amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa imani aliyompa na kuahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu. Amesema pia kuwa amedhamiria kuendeleza diplomasia ya uchumi na kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzani...

*KAMATI YA BUNGE YAPITISHA RANDAMA YA MADINI MWAKA 2026/27*

Image
✅️ Madini Yachangia Asilimia 57 ya Mauzo Yote ya Bidhaa Zisizo za Asili Nje ya Nchi ✅️ Makusanyo mpaka Februari 2026 Yafikia Shilingi Bilioni 880 ✅️ GST Yakidhi Vigezo Kuendelea Kuwa na Ithibati Mpaka 2029 ✅️ Waziri Mavunde Asisitiza Ununuzi wa Helikopta ya Utafiti, Mipango Iko Pale Pale 📍 Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Machi 26, 2026 imepitisha Randama ya Wizara ya Madini kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2026/27 katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma, ambacho pia kimepokea taarifa ya utekelezaji wa Wizara kwa kipindi cha Julai 2025 hadi Februari 2026 kwa mwaka 2025/26. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, ameipongeza Wizara kwa namna inavyosimamia utekelezaji wa majukumu yake yaliyopelekea kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa kufikia asilimia 12.7 katika robo ya tatu ya Julai hadi Septemba 2025, ikiwemo kuibua miradi mipya na shughuli za utafiti,...

MHANDISI MATIVILA AKAGUA MIRADI YA DMDP II, ATOA WITO UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU

Image
📌TARURA kujenga takribani Km. 250 za barabara Manispaa zote za Dar es Salaam ‎ ‎Dar es Salaam ‎ ‎Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amesema Serikali kupitia TARURA inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu mkoa wa Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wake ili idumu kwa muda mrefu. ‎ ‎Ameyasema hayo ‎wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa DMDP II katika Manispaa za Ubungo na Kinondoni, akisisitiza umuhimu wa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati ili kuboresha miundombinu na maisha ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. ‎ ‎Mhandisi Mativila alikagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ya Msumi Km 9.9 na daraja la Msumi na ujenzi wa barabara ya Goba Wakorea km 7.76 zilizopo Ubungo pamoja na ujenzi wa barabara ya Mivumoni Km 4.79 iliyopo Kinondoni ambapo utekele...