MSD YAPEWA SH BIL 642.1 UNUNUZI BIDHAA ZA AFYA.


Deborah Lemmubi-Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeipatia Bohari ya Dawa (MSD) kiasi cha Shilingi Bilioni 642.1 kwaajili ya ununuzi wa bidhaa za afya za, Vituo vya kutolea huduma za afya Nchini.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma Agosti 15,2025  na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bwana Gerson Msigwa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari akielezea masuala ya maendeleo ya Sekta ya Afya Nchini ikiwemo upatikanaji wa Dawa, Vifaa Tiba,Vitendanishi na Usambazaji Dawa kupitia Bohari Dawa akiwa katika Ofisi za Kanda za Bohari ya Dawa Dodoma.

Ambapo pia amesema katika mwaka wa 2024/25 Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 196.3  kati ya bajeti iliyotengwa ya Shilingi Bilioni 299 ikiwa ni sawa na asilimia 98 ya fedha yote ya vituo kwaajili ya ununuzi wa bidhaa za afya.


"Katika kipindi cha miaka minne, Serikali kupitia Wizara Afya imetoa kiasi cha shilingi bilioni 642.1 kwa Bohari ya Dawa (MSD) kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za afya za vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imeweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 196.3 kati ya bajeti iliyotengwa ya shilingi bilioni 200 sawa na asilimia 98 ya fedha yote ya vituo kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za afya. Hii ni fedha nyingi kutolewa katika kipindi chochote tokea kuanzishwa kwa Bohari ya Dawa". 

Aidha Msigwa amesema kuwa MSD imeendelea kuimarisha utimizaji wa mahitaji ya vituo vya kutolea huduma za afya ambapo hadi kufikia mwezi Juni 2025, hali ya utimizaji wa mahitaji ilikuwa asilimia 79 ikilinganishwa na asilimia 39 iliyorekodiwa mwaka wa fedha 2021/22 ambapo Ongezeko hili linatokana na  upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za afya na vituo kuendelea kuwezeshwa kufanya ununuzi wa bidhaa za afya.



 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO