WAZIRI KOMBO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA JICA


Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Bw. Ando Naoki, Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) pembezoni mwa Mkutano wa Tisa wa TICAD uliofanyika jijini Yokohama.

Mheshimiwa Waziri Kombo amepongeza ushirikiano wa Tanzania na Japan kupitia JICA katika ufadhili wa uendelezaji wa sekta za kilimo; nishati; usafirishaji; afya; maji na uendelezaji wa rasilimali watu. 

Katika kikao hicho walikubaliana kuendeleza ushirikiano huo hususan katika sekta za miundombinu bora, uendelezaji wa rasilimali watu; uchumi wa buluu na kilimo, hususan teknolojia ya kuongeza thamani malighafi za mazao.




 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO