HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.
Na,Agnes Mambo Tanga, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk Batilda Burian amesema maendeleo ya taifa hayawezi kupimwa kwa kiwango cha uwekezaji au ujenzi wa viwanda pekee, bali kwa namna serikali na jamii zinavyoweka fursa za usawa wa kijinsia katika ajira, hususan kwa watoto wa kike na wa kiume. Dk Burian ameyasema hayo alipokuwa akifungua maadhimisho ya nne ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake katika Sekta ya Bahari yaliyofanyika jijini Tanga jana (Jumapili) Mei 18/2025. Akimnukuu mwanafalsafa maarufu Plato, aliyewahi kusema kuwa "Kilimo cha jamii yoyote ni jinsi inavyowathamini wanawake", Dk Burian alisisitiza kuwa taifa linapaswa kujipangia malengo ya kuhakikisha usawa wa kijinsia unatekelezwa kikamilifu. "Tusiache mwanamke abaki ufukweni bali tunataka aingie ndani ya bahari," alisema kwa msisitizo.. Alieleza kuwa licha ya juhudi zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali, sekta ya bahari bado inatawaliwa na wanaume, huku takwimu zikionyesha kuwa wanawake wanaofanya ...
Comments
Post a Comment