SEKENKEONE - SHELUI, WILAYA YA IRAMBA KUMEKUCHA KONGAMANO LA WACHIMBAJI WADOGO KANDA YA KATI.
Kongamano hilo litakaloambatana na matembezi ya Amani, linalenga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Madini katika kipindi cha miaka Minne.
Katika miaka hii minne Sekta ya Uchimbaji Mdogo imekua huku mazingira wezeshi yaliyowekwa na Serikali ikiwemo kupatiwa maeneo ya kuchimba, uwepo wa masoko ya madini nchini na masuala mengine yamechangia ukuaji wa shughuli za uchimbaji mdogo ambapo hivi sasa zinachangia asilimia 40 ya makusanyo ya Maduhuli ya Serikali.
Mgeni rasmi ni Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde na litarushwa mbashara kupitia TBC1
*Vision 2030:
Madini ni Maisha na Utajiri*
Comments
Post a Comment