MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TANGA CHAMA CHA NLD AAHIDI KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI WA ZAO LA MKONGE, KUFUFUA VIWANDA,MADINI YA VITO NA UCHUMI WA BLUU,KUONGEZA AJIRA KWA VIJANA
Na,Agnes Mambo,Tanga.
Mgombea kiti Cha Ubunge Jimbo la Tanga Mjini kupitia chama Cha National League for Democracy 'NLD' Ramadhani Salimu amechukuwa fomu ya kuomba ridhaa ya kwatumikia Wananchi Ili kuwaletea maendeleo.
Wakati akichukuwa fomu ya kugombania Ubunge Kwa msimamizi wa uchaguzi ambaye anakaimu nafasi hiyo Afisa uchaguzi Mwanaidi Nondo,mgombea wa chama hicho, amesema atahakikisha masuala ya VIWANDA anatafuta wawekezaji wengi Ili kufufua vilivyokufa na kutambua Madini yanapatikana Kwa wingi kutokana mkoa wa Tanga tumezungukwa na fursa ya Madini ikiwemo Vito.
Aidha zoezi la uchukuwaji fomu katika ofisi ya msimamizi mkuu wa uchaguzi limeanza tokea Agosti 20 hiyo Mgombea wa chama hicho,amechukuwa Agosti 21/2025 Majira ya saa 3:56 katika ofisi ya msimamizi mkuu wa uchaguzi iliyoko halmashauri ya Jiji la Tanga.
Ramadhani amesema endao atapata ridha Kwa Wananchi,wakamchagua atahakikisha anafufua VIWANDA vilivyokufa na kushawishi wawekezaji wengi kuja kuwekeza ikiwemo kufufua zao la kilimo Cha Mkonge.
"Malengo yangu ni kuona Jimbo la Tanga linasonga mbele na vijana wengi wananufaika rasilimali zao Kwani Tanga tuna Madini mbalimbali ikiwemo Vito hivyo,Tanga imebarikiwa tunazao la kilimo Cha Mkonge lakini bado Ile Kasi kama ya miaka ya nyumba haipo ninatamani kuongeza nguvu kama nitapata ridhaa"Alisema Ramadhani.
Akizungumzia ajira Kwa vija amesema imekuwa changamoto kubwa kutokana na ukosefu wa VIWANDA vya kutosha hivyo vijana kuingia katika mikopo ya Kausha damu na kupoteza uelekeo na misingi hasa utafutaji wa rasilimali fedha Ili kujikwamua kiuchumi.
"Endapo nitapata ridhaa ya kwa Wananchi basi kipaumbele changu ni kuondoa vikwazo katika mikopo ya Kausha damu na kuangalia asilimia kumi za vijana,Wanawake,na watu wenye Mahitaji maalum "Alisema Ramadhani.
Amesema Kwa kuwa yeye ni mtaalamu wa ugunduzi wa Dhahabu Madini atahakikisha anaibua vijana watakaoweza kuhakikisha wananufaika na rasilimali zao na kufuta umasikini wa kipato.
Naye Mwenyekiti wa chama hicho wilaya Tanga Mjini Abdulih Karimu amesema Tanga tumezungukwa na Bahari hivyo endapo mgombea wake atapata ridhaa atahakikisha uchumi wa Blue unaimarika na VIWANDA,Zao la kilimo cha Mkonge vinaongezeka na kuwavutia wawekezaji na kutafuta wawekezaji wengi.
Amesema hivi sasa Kasi ya uzalishaji wa zao la Mkonge Iko ndogo tofauti na hapo awali hivyo atakapopata ridhaa Kwa Wananchi na kuchaguliwa ataongeza Kasi na juhudi kubwa zaidi.
Comments
Post a Comment