Mafuwe achukua fomu ya INEC kugombea ubunge Jimbo la Hai

Mafuwe achukua fomu ya INEC kugombea ubunge Jimbo la Hai

Na Musa Mathias,
Moshi, Kilimanjaro. 

Mgombea ubunge mteule kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge kwa kipindi cha pili katika jimbo hilo kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

Agosti 23,2025 Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa (INEC), ilitangaza majina ya wagombea ubunge na uwakilishi kupitia chama hicho, kwa majimbo ya Tanzania Bara na Zanzibar, pamoja na viti maalum kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Mafuwe amekabidhiwa fomu hiyo leo Jumanne , Agosti 26 2025, na Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Aidan Angetile katika Ofisi za uchaguzi zilizopo katika Jimbo hilo.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mafuwe amewashukuru wanachama wa chama hicho kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi kwa mara nyingi kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa kibali, nakishukuru sana chama changu cha Mapinduzi ngazi zote za uteuzi kuanzia Wilaya hadi ngazi ya taifa kwa kuniteua miongoni mwa vyuo wanachama wengi ndani ya Jimbo la Hai, kuwa miongoni mwa kupeperusha bendera ya CCM,"amesema Mafuwe 

Ameongeza"Niwashukuru wale wenzangu ambao tulirejeshwa na chama kuja kuomba ridhaa kwa wanaCCM na wajumbe wa CCM, zaidi nawashukuru sana wanachama wote na wajumbe wote kwa heshima hii kubwa waliyonipa ya kuendelea kuwa Mbunge wao."


"Leo nimekuja rasmi kuchukua fomu ya ubunge Jimbo la Hai, rai yangu kwa wana CCM kuendelea kushikamana, kuendelea kuombea chama chetu, lakini ninayo furaha kuwataarifu Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan alichukua fomu na mimi niliwawakilisha wananchi wa Hai wakati naenda kuchukua fomu pale Dodoma, na mimi sina mashaka kabisa katika Jimbo letu la Hai, tuna jambo naye na yeye anatudai tuna hakika tutapata kura za kishindo kwa kazi kubwa iliyofanyika hapa,"amesema Mafuwe

Amesema "Sisi wanaCCM tukawe wakwanza kuhakikisha uchaguzi wetu unakuwa wa amani na utulivu na haki , sisi Wana Hai tuhakikishe uchaguzi unakuwa wa huru na haki lakini pia kwa umoja wetu tukumbe Wilaya ya Hai inajengwa na wanaHai , amani ya Hai itatunzwa na sisi wenyewe,"

Amesema kila mwana Hai anapaswa kufanya kampeni za kistaarabu kwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.

"Baada ya Oktoba uchaguzi utakuwa umeisha na wataendelea kuwa ndugu, lakini kampeni ziwake na utulivu na amani kila mmoja akimheshimu mwenzake , zaidi kuheshimu kanuni na miongozo iliyotolewa na Tume ya uchaguzi,"amesema Mafuwe 

Naye Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Hai, Aidan Angetile, amewataka wagombea ubunge kusoma na kuzikagua kwa makini fomu walizopewa na Tume ya uchaguzi (INEC) na kuzijaza kwa umakini na kuzingatia muda.

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO