REA KUTEKELEZA KWA VITENDO MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

📌 *Majiko banifu 5,176 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoa wa Iringa* 

📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 14,300 tu* .

📍 *IRINGA* 

Wakati Taifa likiwa kwenye mkakati wa kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi na salama ya kupikia, Wakala wa Nishati Vijijini umekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa  majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku yanayotumia kuni na mkaa mchache sana na yenye ufanisi mkubwa katika matumizi yake.

Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa, Mhandisi Kelvin Tarimo amesema,

Mradi huu umekuja kwa lengo la kuimarisha utunzaji wa Afya za wananchi na Mazingira, kukuza upatikanaji wa Nishati Safi na Endelevu, kupanua usambazaji wa nishati mbadala katika maeneo ya Vijijini na zaidi kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi kupitia teknolojia za kisasa na bora za kupikia.

Mhandisi Tarimo ameendelea kwa kusema, Serikali kupitia wakala wa Nishati Vijijini umeandaa mpango huu wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia ili kufikia lengo la zaidi ya asilimia themanini 80% ya watanzania ifikapo mwaka 2034 wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Mradi huu una gharimu zaidi ya TZS Milioni 296.06 kwa mkoa wa Iringa na unatarajia kufanikisha uuzaji na usambazaji wa majiko banifu 5,176.

Uuzaji na usambazaji wa majiko banifu utafanyika katika wilaya tatu (3) za mkoa wa Iringa, ambapo kwa wilaya ya Kilolo itapata majiko 1,725, wilaya ya Iringa Vijijini majiko 1,725 na wilaya ya Mufindi majiko 1,726.


Mikataba ya mradi huu ilisainiwa tarehe 09 Mei, 2025 kati ya REA na mtoa huduma kampuni ya Greenway Grameen infra Pvt Limited na ECOMAMA Tanzania Limited.

Mtoa huduma atasambaza na kuuza majiko banifu kwa bei ya ruzuku  katika wilaya zote tatu. Gharama ya jiko moja ni TZS 71,500 lakini serikali imetoa ruzuku ya asilimia 80 hivyo mwananchi atanunua kwa gharama ya TZS 14,300 tu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James , ameishukuru na kuipongeza REA pamoja na mtoa huduma kwa kutumia fursa na kuunga mkono juhudi za serikali kwenye matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia na kuongeza kuwa serikali ya mkoa pamoja na wilaya zake itatoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia





 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO